Na Mwandishi Wetu

KUNDI la Muziki wa dansi la Orchestra Sikinde Original, Jumatatu ijayo linatarajia kuachia wimbo wake wa pili mpya uitwao Mchepuko maarufu kama Nyumbani Kumenoga.

Sikinde Original inaundwa na wanamuziki mbalimbali waliowahi kupigia bendi ya DDC Mlimani Park na ambao wengine Bado wanafanya kazi na bendi ya Mlimani Park na bendi zinginezo.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Fatuma Munene amesema wimbo huo unazungumzia Kisa cha wanandoa ambao hawakuwa sawa na kuangukia kwa mchepuko ambapo Bado mambo hayakuwa sawa hadi pale mwenza anapomwambia mwenzie arudi nyumbani Kumenoga.

Munene amesema Sikinde Original ina lengo la kurejesha ladha ile ya Sikinde ya miaka ya nyuma ikachanganya na vionjo vya kisasa.

"Kuna wanamuziki wengi waliopita Sikinde watatumika katika kutengeneza albamu ya kundi hili na katika albamu wimbo wa kwanza ni Mchepuko....huko mbele zipo suprise nyingi sana, tujachojaribu kufanya ni kuinua muziki wa dansi ambao wapo wanaosema umeshuka,"

Katika wimbo huo waimbaji ni wakongwe Bennovilla Anthony, Maximilian Bushoke, Abdalah Hemba, Athuman Kambi na Fresh Jumbe Mkuu. 

Kwa upande wa ala magitaa yamepigwa manne ambapo Solo limepigwa na Omary Seseme, Second Solo, Mkongwe Abdalah Gama, rythim Mjusi Shemboza wakati Bass ni Bonny Chande.

Juma Choka ameshiriki kwenye Drums huku Ibrahim Chande kwenye Trumpet. Huu ni wimbo wa pili kutolewa na Orchestra Sikinde Original. Wimbo wa kwanza ni Sensa ambao ni maalum kuhamasisha zoezi la kuhesabiwa. Video ya Mchepuko iko mbioni kuachiwa pia.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...