Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga ameeleza kwamba maboresho yanayofanywa na mfuko huo hayalengi kumuumiza mwanachama, bali kumulinda kwa lengo la kuimarisha uhai wa mfuko.

Konga ameyaeleza hayo leo Agosti 11,2022 alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari kuhusu taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zinatolewa na baadji ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii na kusababisha taharuki kwa wanachama wa Mfuko huo na Watanzania kwa ujumla.

Ametoa mfano kuwa kama mfuko kwa sasa wanaona kasumba moja ya wagonjwa kwenda hadi hospitali ya taifa ambako wanaamini utaalam wote uko pale, lakini wanaambiwa kesho yake wake wakaonwe kwenye kliniki X. "Mgonjwa anakuwa kwenye hospitali ya Taifa anashushwa na mtaalam yule yule.

"Halafu anaandikiwa vipimo ambavyo anatakiwa arudi akapime hospitali ya Taifa, halafu kesho kutwa anaambiwa utakuja nayo kufuata majibu tutakutana kwenye kliniki Y," alisema Konga na kuongeza "Serikali inachoona ni kwamba kuna vitu ambavyo havijakaa sawa , lakini kikubwa ni usumbufu kwa mgonjwa."

Amefafanua hivyo ndivyo mheshimiwa Waziri aliandika, akisema mgonjwa mmoja vituo vitatu katika siku tatu.

Konga amesema hali hiyo siyo shida kwao wanalipa pale mwanachama anapoenda kutibiwa, lakini wanaangalia usumbufu ambao mgonjwa anapata.,kwa hiyo ndiyo maana wakasema mtu akishafika Hospitali ya Taifa wanaamini pale ndipo penyewe wasimuone kesho anarudi huko chini.

Aidha amesema sio kweli kuwa ukishaenda hospitali moja utatibiwa hospitali hiyo hiyo. "Jamani sisi sote ni Watanzania, leo nimetoka Dodoma nikiumwa hapa Dar es Salaam natakiwa nitibiwe hapa hapa, kesho (leo) narudi Dodoma nikiumwa nirudi tena kutibiwa Dar es Salaam! Kitu ambacho hakiwezekani," amesema na kuongeza kwamba hauwezi kuwa na udhibiti wa namna hiyo na hayapo hayo kwenye miongozo yao.

Konga amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa NHIF mwaka 2001, wamekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau wake ili kujadili na kupanga kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zinazojitokeza ili kuboresha huduma kwa wadau wote.

"Utaratibu wa kukutana na wadau (watoa huduma, waajiri na wanachama) umekuwa na manufaa na umeweza kuboresha huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanufaika.Hivyo, kabla ya kufanyika kwa mabadiliko katika mfumo wa bima ya afya, Mfuko umekuwa ukiwashirikisha wadau hatua zote ili kuwa na uelewa wa pamoja wakati wa utekelezaji.

"Hata hivyo, Mfuko utaendelea kuwashirikisha zaidi wadau wake ili kuepusha sintofahamu inazoweza kujitokeza," alifafanua Konga na kufafanua kuwa hata hivyo, kwa sasa Serikali ipo hatua za mwisho kuimarisha mfumo wa ugharimiaji wa huduma za afya kupitia mfumo wa bima ya afya.

Akizungumza kuhusu ukomo wa siku za kutibiwa, ameeleza kwamba ema hayo ndiyo yaliyoleta taharuki kutokana na kupotoshwa kwani hakuna ushahidi kuna mtu aliyeugua ndani ya siku moja akahama akakutana na hiyo changamoto.

Ameweka wazi katika kuhakikisha wanachama wanaostahili kupata huduma wanatambulika, mfumo wa utambuzi wa wachangiaji na wategemezi umeimarishwa ili kuondoa wategemezi wasiostahili. "Mathalani, katika miaka ya awali, baadhi ya wanachama waliandikisha majirani, shangazi, mjomba, dada wa kazi nk kama wategemezi na baadhi ya wanachama waliuza nafasi zao kwa watu wengine."

Konga amesema hali hiyo inasababisha uwepo wa wategemezi wasiostahili, hivyo kuwanyima haki wategemezi wanaostahili. Pia, katika siku za hivi karibu kumekuwa na maombi mengi ya wanachama ya kutaka kutoa kundi hili.

"Katika kuhakikisha kundi la wategemezi wasiostahili wanakuwa na fursa ya kuendelea kupata huduma, kundi hili linaweza kujiunga kupitia utaratibu wa vifurushi vya bima ya afya," amesema na kuongeza ili kuhakikisha wanachama wa Mfuko wanapata huduma bora za matibabu, Mfuko umeweka utaratibu wa kufanya maboresho katika kitita chake cha Mafao yatolewayo kwawanachama wake na kwamba kwa mara ya mwisho maboresho ya Kitita cha Mafao yalifanyika mwaka.

Mkurugenzi MKuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya( NHIF) Bernard Konga akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu maboresho yanayofanywa na Mfuko huo

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...