*Atoa ahadi kwa Lindi Jumbo Ltd kuwakutanisha na mabenki
*Aweka msisitizo kushiriki Sensa ya Watu na Makazi
Na Mwandishi wetu,Lindi
NAIBU
Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameahidi kuikutanisha Kampuni ya
Lindi Jumbo Limited inayotarajiwa kuanza uchimbaji wa madini ya Kinywe
(Graphite) hivi karibuni na taasisi za fedha kwa lengo la kupatiwa mkopo
ili ianze uzalishaji wa madini hayo kwa wakati.
Dkt.
Kiruswa ametoa ahadi hiyo baada ya kutembelea eneo la kijiji cha
Matambarale panapo jengwa mgodi wa uchimbaji madini hayo katika wilaya
ya Ruangwa mkoani Lindi.
Dkt.
Kiruswa amesema, Wizara ya Madini imeingia mkataba na mabenki
mbalimbali kwa lengo la kutoa mikopo kwa wachimbaji na wafanyabiashara
ya madini ambapo ameahidi kuikutanisha Kampuni hiyo na mabenki.
"Mhe.
Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametuagiza sisi Wizara ya Madini
kuwalea na kuwaongoza wachimbaji wa madini ili muweze kufanya shughuli
zenu kwa tija, hivyo wiki hii nitazungumza na mabenki ili waone jinsi
gani wataweza kuwapatia mkopo muanze uzalishaji wa madini haya muhimu,"
amesema Dkt. Kiruswa.
Aidha,
Dkt. Kiruswa amesema kuwa, Wizara ya Madini imefungamana na sekta
nyingine ambapo ameahidi kukutana na Wizara ya Maji, Nishati na
Miundombinu kwa lengo la kutafuta suluhisho la upatikanaji wa maji,
umeme na barabara katika maeneo yanayotarajiwa kuanza uzalishaji wa
madini ya Kinywe (Graphite).
Pamoja
na mambo mengine, Dkt. Kiruswa amesema lengo la ziara yake hiyo ni
kutaka kujua maendeleo ya Sekta ya Madini katika mkoa wa Lindi na kujua
changamoto zinazoikabili sekta hiyo mkoani humo.
Pia,
Dkt. Kiruswa ametembelea eneo linalotarajiwa kujengwa mgodi wa kuchimba
madini ya Kinywe na kiwanda cha betri cha Uranex kilichopo wilayani
Ruangwa ambapo amekagua ujenzi wa nyumba 59 zinazojengwa kwa ajili ya
makazi ya waliopisha eneo la mradi huo ambapo ameonesha kuto ridhika na
ujenzi huo.
Awali, Dkt.
Kiruswa alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma pamoja na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kwa lengo la kupata taarifa
za shughuli za uchimbaji madini katika mkoa huo.
Aidha,
Dkt. Kiruswa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wachimbaji wa madini
kote nchini kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ili
kufanikisha zoezi la kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya
Madini na Taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma amempongeza Dkt.
Kiruswa kwa kufanya ziara yake mkoani humo ambapo amesema ana uhakika
changamoto zinazo ikabili Sekta ya Madini mkoani humo zitapatiwa
suluhisho.
Naye, Meneja
Uhusiano wa Lindi Jumbo Limited Paul Shauri amesema, mgodi huo ukianza
uzalishaji utazalisha zaidi ya tani 39,000 za graphite kwa mwaka
ambapo maisha ya mgodi yanatarajiwa kuwa miaka 24 na una hifadhi ya
zaidi ya tani milioni 300 za graphite zenye ubora wa hali ya juu .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...