Mkurugenzi wa wateja binafsi kutoka benki ya Nbc Elibariki Masuke akizungumza mara baada ya kutambulishwa rasmi Kwa Shindano la ''Nbc Lugalo patron trophy " lengo likiwa ni kumuaga aliyekua Mlezi wa Klabu ya jeshi ya Lugalo gofu Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo na kumkaribisha rasmi Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda linalotarajiwa kufanyika agosti 27 mwaka huu katika viwanja vya jeshi lugalo gofu Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo gofu Michael Luongo akishikana mikono na Mkurugenzi wa wateja binafsi kutoka benki ya Nbc Elibariki Masuke pamoja na zawadi itakayotolewa Kwa Mshindi wa jumla

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KLABU ya Jeshi ya Lugalo gofu limeandaa Shindano la "Nbc Lugalo patron trophy" kumuenzi Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali Venance Mabeyo linalotarajiwa kufanyika Agosti 27 mwaka huu katika viwanja vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Lugalo Dar es Salam.

Akizungumzia ujio wa shindano hilo Mwenyekiti wa Klabu Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luongo amesema Lengo la shindano hilo ni kumkaribisha mlezi mpya wa klabu hiyo ambaye ni mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda.

Hata Luongo ameongeza kuwa Mgeni rasmi katika kufunga shindano hilo ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kushuhudia makabidhiano hayo mapya kwa Mlezi wa Klabu hiyo kwani ni Moja ya wadau wa Sekta ya Michezo hivyo italeta chachu kubwa Kwa mchezo wa gofu kupata hamasa zaidi.

Pia amesema Shindano litajumuisha wachezaji kutoka klabu mbalimbali kama Kilimanjaro, Morogoro gymkhana pamoja na gymkhana ya Dar es salaam.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Benki ya NBC ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo Mkurugenzi wa Wateja binafsi na Wateja Wadogo Ellibariki Masuke ameishukuru Klabu ya Lugalo Gofu kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo na amewaomba wadau na Watanzania wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo.

Benki ya NBC imekabidhi vifaa vya Mchezo wa Gofu ambavyo vitatumika katika shindano hilo,"NBC Lugalo Patron Trophy'" linarotarajiwa kufanyika 27 Agosti 2022, ambapo mgeni rasmi katika ufungaji wa Shindano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa utamaduni,Sanaa na Michezo Mohammed Mchengelwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...