RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Kenya, ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametoa taarifa ya awali ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya leo  Agosti 11, 2022 jijini Nairobi, Kenya.

Katika taarifa hiyo, ameeleza kuwa Timu ya uangalizi imeshuhudia uchaguzi kufanyika kwa utulivu, uhuru na amani na kuwapa Wakenya fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha amesema kuwa anaamini mchakato uliobaki utafanyika kwa haki kama ambavyo uchaguzi umefanyika ili kuendana na vile wananchi wa Kenya wameamua kwenye sanduku la kura.

Ameomba Wakenya waendelee kuwa watulivu sasa na hata baada ya matokeo kutangazwa.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Kenya, ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, amekutana na kufanya mazungumzo na Mgombea Urais wa Kenya, George Wajackoyah  kutokea chama cha RPK.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...