Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media, Nengida Johanes akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Agosti 10, 2022 kuhusiana na Tamasha la Twende zetu kwa Yesu litakalofanyika Agosti 13 katika uwanja wa Uhuru. Kushoto ni Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Redenta Nyahonge na Kulia ni Msimamizi wa Vipindi Upendo Media, Upendo Tuheri.
Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Redenta Nyahonge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Agosti 10, 2022 kuhusiana na Tamasha la Twende zetu kwa Yesu litakalofanyika Agosti 13 katika uwanja wa Uhuru. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media, Nengida Johanes.


Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media, Nengida Johanes, Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media, Nengida Johanes na Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Redenta Nyahonge wakionesha Tisheti zitakazovaliwa katika siku ya Tamasha la Twende Zetu kwa Yesu litakalofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Agosti 13,2022.


NYOTA wa Nyimbo za Injili kutoka Afrika Kusini, Zaza Mokheti na Rose Mhando kutumbuiza katika Tamasha la 'Twenzetu kwa Yesu' lililo andaliwa na Upendo Media ya Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), linalotarajiwa kufanyika Agosti 13, 2022 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Agosti 10, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media, Nengida Johanes amesema waimbaji mbalimbali watatumbuiza tamasha hilo. 

Amesema kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Malasusa atafungua tamasha hilo. Likiwa na Kauli mbiu ya 'WA ZAMANI SI WASASA'. 

Nengida amesema tamasha hilo litakuwa na wanenaji mbalimbali ambao watanogesha tamasha hilo akiwemo Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Tabora, Agrey Mwanri, Mchungaji Msaidiziwa Dayosisi ya Mashariki, Deogratius Msanya. 

Amesema kuwa Vijana zaidi ya 2500 watahudhuri tamasha hilo na watatoka pia katika nchi ya Rwanda, Kongo na Uganda.

Waimbaji na kwaya mbalimbali zitakazotumbuiza katika Tamasha hilo ni Rehema Semfukwe, Hyper Squad, Yamungu Mengi (Komando wa Yesu), Kwaya ya AIC Chang’ombe, The Survivor Kwaya ya Efatha Morovian, Essence of Worship, Praise Team ya KKKT, DMP Jimbo la Magharibi, Kwaya ya Vijana KKKT Usharika wa Vituka, Kwaya ya Uinjilisti Haleluya ya KKKT Usharika wa Mbezi Beach, Kwaya ya Vijana Mabibo Farasi, Kwaya ya Vijana KKKT Kitunda Relini na Kwaya ya Vijana KKKT Kinyamwezi.

Akizungumzia kuhusiana usalama na Ulinzi wa siku hiyo Nengida amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke limejipanga kuhakikisha tamasha hilo linafanyika kwa amani na Utulivu. 

Aidha Nengida amewakaribisha vijana wote hapa nchini kuhudhuria tamasha hilo kwa kiingilio cha shilingi elfu tano (5000) na tamasha hilo litaanza saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Upendo Media wamekuwa waandaaji wa Tamasha la Twenzetu kwa Yesu mara tisa mfululizo likigusa maisha ya Vijana wa aina zote sio wakristo tu bali ni la watu wa imani zote.

Kwa Upande wa Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Redenta Nyahonge amewahakikishia wananchi na watakaohudhuria tamasha hilo kuwa kutakuwa na ulinzi wa Kutosha na Usalama licha ya kuwa na Mechi ya Simba  na Yanga saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...