Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Kaliua

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amepokea malalamiko mbalimbali ya wananchi wa Kijiji cha Ibambo wilayani Kaliua mkoani Tabora na miongoni mwa malalamiko hayo ni kukithiri kwa mimba kwa wanafunzi wa kike.

Amepokea malalamiko hayo leo Agosti 16 mwaka huu akiwa wilayani Kalia ambako amefika kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020/2025.

Baada ya kuwasili Kaliua Shaka alieleza lengo la ziara yake lakini alitoa nafasi kwa wananchi kutoa changamoto zao ambapo moja ya changamoto ni kukithiri kwa mimba kwa wanafunzi wa kike.

Kutokana na malalamiko hayo Shaka alimtaka Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Gilbart Kalima kutoa maelekezo ya Chama kuhusu hali hiyo ambapo amesema lazima jamii kubadili mienendo na kwamba mtoto wa kile ni mali ya Serikali.

“Watoto wa kike ni mali ya Serikali, wanatakiwa waache wasomwe watimize malengo yao , kuwapa mimba watoto wa shule ni kosa kisheria.”Nimesikia kuna baadhi ya walimu wanahusishwa  kuwapa mimba wanafunzi hili ni kosa kisheria, watafutwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.”

Aidha amesema kuna kila sababu ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kujenga maadili katika jamii kuondokana na vitendo ambavyo havina tija.



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Gilbart Kalima akizungumza mbele ya Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...