*Ataja mabilioni ya fedha yaliyotengwa kufanikisha mpango huo

*Ataka wananchi wote kumpongeza na kumuunga mkono kila hatua


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan amesimama kidete kuhakikisha anaifungua nchi kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Shaka amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi Ushokola wilayani Kaliua mkoani Tabora ambapo alifika kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 2.7 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

“Nataka kuchukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo watanzania , mmenituma nije nikague barabara hii inayojengwa hapa Kaliua.Kwenye Wilaya hii Rais Samia ndani ya kipindi kifupi sana cha uongozi wake anakwenda kujenga barabara kilometa 10.

“Jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi imepata uhuru na kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya Wilaya hii Rais Samia ndio anajenga barabara za lami. Anawajengea barabara lakini wakati huo huo anawawekea na taa inamaana Kaliua inakwenda kuwa ya kileo,”amesema Shaka.

Ameongeza kuwa “Kwa hiyo wote kwa pamoja tumpongeze Rais Samia , tumekuwa mashuhuda namna Rais Samia amesimama kidete kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini uchumi wa kikanda na uchumi wa kimaeneo.

“Kukamilika kwa barabara hizi kilometa 10 ni hatua mpya ya kufungua uchumi wa wana Kaliua.Mtasafirisha mazao lakini mtarahisisha maisha yenu ya kila siku kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi zaidi.

“Kazi hii sio kazi ndogo kumpata Rais mwenye maarifa , mwenye mawazo lakini kupata Rais ambaye anafikiria wananchi wake wanahitajia nini na kwa wakati gani,”amesema Shaka.

Amefafanua ni jambo la kumshukuru Mungu, tunaye Rais anayejua wananchi wake wanataka nini , lakini tunaye Rais ambaye kwa wakati huu anajua wana Tabora wanahitaji nini.

“Tunaye Rais anayejua wana Kaliua wanataka nini , hasa kuliona hilo kwa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan nadhani wote mmesikia amesaini mikataba 10 kwa niaba ya mikataba 968 ambayo inakwenda kujenga barabara za kisasa kabisa.

“Anakwenda kufungua miundombinu ya barabara nchi nzima, mikataba hiyo fedha ni nyingi mno zinazokwenda kutumika zaidi ya Sh.bilioni 248 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara ndani ya nchi yetu.Niwaombe wananchi itakapokamilika barabara hizo tutunze ili ziishi kwa muda mrefu,”amesema.

Amewaomba wananchi wote kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia njema aliyokuwa nayo akitoa mfano kwamba Kaliua wameanza kuona maajabu.“Kaliua mlitegemea kuyaona haya nani kama Rais Samia, kwa hiyo maendeleo haya naomba myathamini sana. 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na Wananchi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akisoma baadhi ya Nyaraka zilizowasilishwa kwake na mmoja wa Wananchi  kwenye mkutano wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akimvisha kanga ya Nyamitwe Maganga mkazi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Shaka akisikiliza kero kutoka kwa Nyandwi Dubo (aliyeshika vipazasauti) huku wananchi wakifuatilia mkutano katika Kijiji cha Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

Shaka akicheza Ngoma yenye asili ya Wanyamwezi katika Kijiji cha Ushokola, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...