Meneja wa Kiwanja cha Ndege Songwe  wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege (TAA) Mhandisi Danstan Komba akizungumza na waandishi habari kuhusiana fursa zilizopo kwenye kiwanja hicho kwenye maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yaliyofanyika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Afisa Biashara na Masoko wa  Antony Kipopota  akiwahudumia wananchi waliotembelea banda hilo  hicho kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yaliyofanyika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Kushoto ni Afisa uhusiano TAA, Mariam Lussewa.
Afisa Mipango na Takwimu Edward Kimaro akiwahudumia mwananchi aliyetembelea banda hilo  hicho kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yaliyofanyika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege(TAA) imesema kuwa kiwanja cha ndege Songwe mkoani Songwe kuwa kitovu kwa Nyanda za Juu Kusini kwenye usafirishaji wa matunda na mboga mboga kwa kutumia usafiri wa ndege kwenda nje kwa ajili ya masoko.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Meneja wa Kiwanja cha Ndege Songwe mkoani Songwe Mhandisi Dunstan Komba amesema serikali inatarajia kuleta ndege za mizigo ambapo itakuwa rahisi katika kuchochea kilimo cha matunda na mboga mboga kwenda katika masoko ya nje.

Komba amesema kuwa kiwanja cha ndege Songwe kina eneo kubwa ambapo watu wanaweza kuwekeza kwenye hoteli , Maghala yakuhifadhia Bidhaa za Mbogamboga na Matunda (Parachichi) pamoja kujenga majengo makubwa ya kutoa huduma mbalimbali (Mall)

Aidha amesema kuwa hadi sasa usafirishaji wa mizigo katika kiwanja hicho matunda na mboga mboga ni sehemu ya mizigo inayosafiri na ndege.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...