Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Jafari Semkiwa (kushoto) akipokea cheti cha Ushindi wa pili kitaifa kwa Kundi la Kampuni za Mawasiliano walichoshinda katika kilele cha Maonesho na Sherehe ya Nanenane yaliofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) walioshiriki kwenye Maonesho ya Nanenane mkoani Mbeya wakifurahia tuzo ya ushindi wa pili kwa Kundi la Kampuni za Mawasiliano Kitaifa katika kilele cha Maonesho na Sherehe ya Nanenane yaliyofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Onesmo M. Buswelu na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mhe. Gilberto Sanga wakitembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Wakulima Kitaifa Nanenane Mkoani Mbeya ambapo wamepongeza juhudi zinazofanywa TTCL katika kutoa huduma mbalimbali na hasa kampeni mpya ya Faiba Mangoni Kwako.



Baadhi ya wananchi wakipata huduma mbalimbali ndani ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Wakulima Kitaifa Nanenane Mkoani Mbeya.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetwaa ushindi wa pili kwa Kundi la Kampuni za Mawasiliano Kitaifa katika kilele cha Maonesho na Sherehe ya Nanenane yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

TTCL imetangazwa mshindi leo katika kilele cha sherehe hizo za maonesho ya Nanenane huku nafasi ya mshindi wa pili kitaifa ikichukuliwa na kampuni ya Simu ya Halotel Tanzania.

Akizungumza katika Banda la TTCL, Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Mujuni Kiyaruzi, amewashukuru Watanzania waliopata fursa ya kuwatembelea katika Banda la TTCL kwenye maonesho ya Nanenane mwaka huu Viwanja vya John Mwakangale na wateja wote wanaoendelea kuwaunga mkono.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Mujuni Kiyaruzi, akionesha tuzo ya ushindi wa pili kwa Kundi la Kampuni za Mawasiliano Kitaifa iliyotwaliwa na TTCL katika kilele cha Maonesho na Sherehe ya Nanenane jijini Mbeya.

Amesema Shirika la Mawasiliano Tanzania limedhamiria kumsaidia mkulima, kuendesha kilimo biashara kwa manufaa hasa kupata taarifa sahihi za masoko kupitia sekta ya mawasiliano ili ziweze kusaidia kupata masoko na hatimaye kukuza kilimo nchini.

"Mwaka huu 2022 tupotena kwenye viwanja vya John Mwakangale Maonesho ya Nanenane sisi TTCL kwa ajili ya kuwafikia wananchi, lakini kwa sababu hizi ni Siku Kuu za Wakulima tumewalenga hasa wakulima na kauli mbiu ya mwaka huu ajenda 1030 kilimo ni biashara na tunapozungumzia biashara hakuna namna utazungumzia biashara bila kuzungumzia uchumi wa kidijitali.

Na sisi kama shirika kubwa la mawasiliano tunawaunganisha wakulima na masoko lakini pia na taarifa zinazohusu mahitaji yao ya kilimo yalioko duniani kwa njia ya mawasiliano ya mtandao na mawasiliano ya simu," alisema Mhandisi Kiyaruzi.

Naye Afisa Mauzo TTCL Mkoa wa Mbeya, Bi. Ida Yesaya alisema wananchi wataofanikiwa kutembelea banda hilo watapata huduma zote kama vile huduma ya mihamala kupitia simu (T-Pesa), huduma za simu za mezani zisizotumia waya, huduma za simu za mkononi na huduma za vifurushi vyote vya simu vya kampuni ya TTCL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...