Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kaliua


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema kuna haja ya kufuatilia mfumo wa malipo ya Serikali ambao umekuwa ukitumika kama kisingizio cha kukwamisha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 16 wilayani Kaliua mkoani Tabora baada ya kupokea taarifa ya kukwama kwa ujenzi wa mradi wa bwawa la maji Ichemba na hivyo kuendelea kusambaza changamoto ya uhaba wa maji.

Shaka amesema mfumo usiwe kisingizio cha kukwamisha shughuli za maendeleo za wananchi."Msitumie mfumo kama kisingizo cha urasimu kukwamisha shughuli za wananchi

“Tunakwenda kufuatilia tuambiwe shida nini, haiwezekani mfumo mwezi mzima haufunguki? Hawa wananchi ukiwaambia mfumo haufunguki watakuelewa lakini mimi sikuweli

"Kwa sababu kwanza simaini huo mfumo mwezi mzima usifunguke, siamini hata siku moja, sasa tutakwenda kufuatilia kwanini kumekuwa na urasimu.Masuala muhimu na msingi yanayogusa maisha ya wananchi hawa.

“Na huo urasimu unatokana na huo mfumo kwamba mwezi mzima haufunguki au unatokana na nini? Na kama ni urasimu wa mfumo tutashauria Serikali kuboresha mifumo yake ili kuendana na kasi na spidi ya maendeleo ya Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema Shaka.

Aidha amefafanua mbele ya wananchi wa Wilaya ya Kaliua jimboni Ulyankulu kuwa amemsikia Waziri wa fedha wakati anasaini mikata ya TARURA mbele ya Rais, alisema Rais anapotoa fedha zikachelewa kutoka huo anafutilia mara kwa mara.

Shaka amesema sasa kule juu Rais anafuatilia hivyo ameelekeza na kwenye ngazi za chini anataka kuona ufuatiliaji wa karibu ili mikwamo hiyo iwe inakwamuka na wananchi wafaidike na miradi ya maendeleo inayotolewa na Rais Samia Suluhu Haasan ambayo inawagusa wao moja kwa moja.

Awali Mhandisi wa Wakala wa Maji Vijijini ( RUWASA ) amesema wamejenga mradi wa maji Kanoge kwa ajili ya kuhudumia vijiji viwili vya Kanoge na Ichemba na tayari huduma imeanza kutolewa lakini changamoto ni gharama za uendeshaji kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta.

"Jumuiya ya maji imekuwa ikitumia jenereta kwa ajili ya kuendesha mitambo,hivyo wanatumia mafuta ambayo kwa sasa bei Iko juu.Tumeshaongea na TANESCO kwa ajili ya kutupatia umeme hivyo wameshatupa a namba ya milipo( Control nomber na tutalipa kabla ya mwishoni mwa mwezi huu.

"Kwa mujibu wa malipo ya Serikali mfumo ukishafunguliwa wanalipa mambo mengine yanaendelea,wametuambia wenzetu kuwa ndani ya mwezi wa Nane malipo yanafunguliwa na tutalipa.

Aidha amesema katika kutatua changamoto ya maji , bwawa la Ichemba litakapokamilika litaondoa adha ya maji na kwamba wanaamini bwawa hilo litakuja msada mkubwa kwa wananchi wa Jimbo la Ulyankulu.

"Tayari imeshatangazwa na mchakato wa manunuzi tumeshapata tathmini na wenzetu juzi tumekwenda wametuambia tukimaliza kuchambua mkandarasi mwenye sifa ujenzi tutaanza. Mradi huu ulianza mwaka 2018.

"Ila changamoto iko kwenye upatikanaji wa fedha, maana tulifanya usanifu lakini fedha sasa michakato ya kutangaza tenda haikufanyika, tayari fedha litengewa Sh. zaidi ya bilioni 3.7 kwa hiyo mchakato ukikamilika na mwanasheri akiidhinisha mkandarasi ataingia kazini kuanza ujenzi , mradi huo ukishakamilika utasaidia kuhudumia kata tisa."








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...