Na. Edmund Salaho/TANAPA

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA ) limeshiriki maonesho ya Nanenane 2022, ambayo yamehitimishwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo  Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, William Mwakilema alipata fursa ya kueleza pamoja na mambo mengine jinsi Uhifadhi na Utalii unavyochangia kwenye ajenda ya kilimo 10/30 yenye lengo la kuwainua wakulima nchini kwa asilimia 10% kufikia 2030 lakini pia alihamasisha watanzania kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa masilahi mapana ya mipango endelevu ya nchi yetu

Aidha, Mwakilema alibainisha jinsi shirika linavyoendelea kuunga mkono juhudi alizozianzisha Rais za kutangaza utalii kupitia filamu maarufu duniani ya “The Royal Tour” kwa kuhamasisha na kutangaza vivutio ndani na nje ya nchi ambapo matokeo ya Royal tour yameanza kuonekana kwa mafuriko makubwa ya wageni katika hifadhi zetu.

“Mhe.Rais kwa mwezi julai 2021, mwaka wa fedha uliopita tulipata watalii tisini na mbili elfu, ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha julai 2022 mwezi mmoja uliopita tumepata watalii zaidi ya laki mbili na thelathini na tano elfu ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia mia moja na hamsini na tatu na ongezeko la mapato kwa mwezi huo tumepata kiasi cha zaidi ya billioni arobaini na saba” alisema Kamishna Mwakilema.

Pia, Mwakilema alibainisha namna shirika lilivyojipanga katika kufikia lengo la serikali la kufikisha watalii millioni tano, na mapato ya fedha za kigeni zipatazo dolla za kimarekani billioni sita ifikapo 2025

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania( TANAPA) limekuwa mdhamini mkuu wa maonesho ya Nanenane chini ya wizara ya kilimo ili kuendeleza na kuhabarisha umma jinsi Utalii na Uhifadhi unavyoweza kuchangia katika kuhakikisha Taifa linatekeleza kikamilifu ajenda 10/30 kwani mnyororo wa thamani ya utalii utachangia kuongezeka kwa soko la bidhaa za kilimo,ufugaji, uvuvi kwani idadi ya watalii wanavyoongezeka kuingia nchini ni dhahiri watahitaji chakula kinachozalishwa kupitia sekta hii ya kilimo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...