Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa amesema Taasisi yake imeanza rasmi jukumu la kusimamia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022 – 2023 ya Shilingi Bilioni 361.5 na nyongeza ya shilingi Bilioni 71 kutoka kwa wafadhili na mikopo midogo hivyo kuitimisha jumla ya shilingi Bilioni 432 zitakazotumika kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji nchini ikiwemo skimu 21 na mabwawa 14 ya umwagiliaji katika baadhi ya skimu zitakazojengwa chini ya Wizara ya Kilimo.

Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Nane nane (John Mwakangale) jijini Mbeya mara baada ya kutiliana saini mikataba ya makubaliano ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na kampuni 17, Bw, Mndolwa amesema jukumu la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kutekeleza ujenzi wa zaidi ya hekta 95 elfu za umwagiliaji na kwa mujibu wa maagizo ya serikali pamoja na ilani ya chama tawala kuhakikisha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 1,200,000 mwaka 2025.

Hivyo tume inajukumu la kujenga miundombinu hiyo kwaniaba ya serikali na kuwaelimisha wakulima mbinu bora za kilimo cha umwagiliaji pamoja na kuwapa wakandarasi maeneo ya kujenga skimu na mabwawa pamoja na kuwasimamia ili wajenge miradi hiyo kwa ufanisi unaotakiwa.

“Ni wahakikishie watanzania kuwa tutatekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakuwa endelevu.”

Bw, Mndolwa ameongeza kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekuja na mpango wa (Block farming) wenye lengo la kufungua mashamba makubwa na kuwapa vijana walime kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika shughuli za kilimo biashara, hivyo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaandaa mashamba hayo mkoani Dodoma na utafuatiwa na mkoa wa Mbeya na kisha mikoa mingine nchini.

“Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan anataka kuwaona vijana, nguvu kazi ya taifa hili iende kwenye uzalishaji isiende kwenye kuuza vitu vidogo vidogo, kijana anaweza kuwa na Bodaboda na akatumia bodoboda yake kwa shughuli za shamba na abiria katika muda wa ziada.”

Kwakufanya hivyo nchi itakuwa na chakula cha kutosha na vijana watakuwa na ajira, hivyo kuitimisha agenda 10/30 ya kilimo ni biashara.

Bw, Mdolwa ametumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza fedha nyingi katika sekta ya umwagiliaji pamoja na watendaji wakuu Wizara ya Kilimo kwa kumuunga mkono hivyo kurahisha utendaji wake.



Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua utekelezaji wa shughuli za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika maonyesho ya Nane nane viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.Aliyevaa kofia ni Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe,Kushoto kwa Mheshimiwa rais. Samia Suluhu Hassan ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa.


Block Farm – Mradi wa Shamba la vijana Chinangali – Mkoani Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kushoto jukwaa kuu) na wageni waalikwa wakishuhudia utilianaji saini mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji Skimu ya Mbaka ( Mbeya ) baina ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Mkandarasi - KIKIM. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi wa Kampuni ya KIKIM Mhandisi Mhonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...