Njombe


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameshangazwa na baadhi ya hospitali kuwatoza wagonjwa kiasi cha shilingi elfu 15,000 ili kuweza kumuona daktari jambo ambalo sio sawa na kuahidi kuchukua hatua ili kupunguza gharama zisizo za lazima kwa wananchi.

Waziri Ummy amebainisha hili mkoani Njombe wakati Rais Samia akikagua jengo la mama na mtoto katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Njombe na kuwahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kuimarisha huduma za afya.

“Nimeona tatizo moja kumuona daktari ni Shilingi elfu kumi na tano hapana,hii ni ya nini? Kwasababu daktari tunakulipa mshahara, kwa hiyo hili nalifanyia kazi nchi nzima”Amesema Waziri Ummy

Amesema serikali itahakikisha inapunguza gharama zisizo za lazima kupata huduma bora za afya na tayari timu ya wataalamu imeshaanza kufanya kazi kwa kuwa serikali inapowaomba Wananchi kuchangia haina lengo la kuwakomoa.

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe inajumla ya majengo matano hadi sasaikijumuishwa na jengo la mama na watoto ambale linataraji kulaza zaidi ya wagonjwa 150 kwa siku na kufanya ukamilifu wa Shilingi bilioni 25 zilizotumika fatica ujenzi wa hospital hiyo ulio anza tangu Mwaka 2016.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...