Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO  la Wanasayansi Chipukizi (YST) limesema mwaka huu wa kwa mwaka huu 2022 imepokea idadi kubwa ya maombi ya kazi za kisayansi kutoka kwa wanafunzi wanaomba kushiriki mashindano ya sayansi  yanayofikia 1,143 na yatafanyika kwenye kila mkoa.

Akizungumza leo Mwanzilishi Mwenza wa YST 

Mwanzilishi Mwenza YST Dkt.Gozibert Kamugisha amesema ongezeko la maombi ni sawa na asilimia 92.4 kwa idadi ya kazi za kisayansi zilizowasilishwa ikilinganishwa na mwaka  2021.

"Ongezeko hilo ni ni ishara kuwa programu ya YST imepokelewa vizuri na kustawishwa katika mikoa ambapo mamlaka za mikoa zimeshiriki kikamilifu katika uendeshaji wa programu hii. Mwaka huu maonesho ya Kisayansi yatafanyika katika kila mkoa na yamepangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

"Kazi za kisayansi 336  zitaoneshwa katika mikoa mbalimbali lakini idadi ya kazi za Kisayansi zisizopungua sita zenye ubora zitachaguliwa kutoka kila maonesho ya mkoa ili zishiriki katika maonesho ya kisayansi ya kitaifa yaliyopangwa kufanyika Desemba 8,mwaka 2022."

Amefafanua kwenye Maonesho ya 2021, maombi 594 ya kazi za sayansi yaliwasilishwa na wanafunzi kwa YST ambapo kazi za sayansi  204 zilikubaliwa kushiriki maonesho ngazi ya mikoa na kutoka ngazi ya mikoa kazi za sayansi 172 zilichaguliwa kushiriki  maaonesho  ya kisayansi kitaifa

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland ameeleza wamekuwa wafadhil wa kujivunia na taasisi ya Young Scientist Tanzania (YST) kwa miaka 12 mfululizo, ikiwa ni pamoja na kutoa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi wote washindi wa YST kwa watakaosoma na kuhitimu  masomo yao ya Chuo Kikuu baada ya kumaliza masomo yao ya elimu ya juu.

Ameongeza mpaka sasa Karimjee imeshadhamini wanafunzi 37 kufikia mwaka 2021 na itaendelea kudhamini huku akisisitiza  pia wanafunzi wanne watakaoshinda mwaka huu itafanya kufikia idadi ya wanafunzi 41 hadi mwaka 2022.

Amesema kwa miaka 12 Karimjee Foundation imekuwa ikitoa mkono wa uhisani kwa YST,  na kwamba walianza na shule 4  mwaka 2011, mpaka  kufikia kuwa na  maonesho ya kitaifa na sherehe za Tuzo kitaifa pia. "Tumeweza kufikia shule zote za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani."Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania Young Scientists Tanzania (YST) Dr Gozibert Kamugisha (kushoto) akizungumza na wanahabari kuhusu namna Taasisi hiyo ilivyoweza kuinua hamasa ya wanafunzi kupenda sayansi kwa vitendo kupitia mafunzo mbalimbali yanayotolewa mashuleni na Taasisi hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) Caren Rowland ambayo ndio mdhamini Mkuu wa YST.Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania Young Scientists Tanzania (YST) Dkt. Gozibert Kamugisha (kushoto)  akisisitiza jambo Kulia ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) Caren Rowland ambayo ndio mdhamini Mkuu wa YST.Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) leo katika ukumbi wa  Hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania Young Scientists Tanzania (YST) Dr Gozibert Kamugisha (hayupo pichani)
Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland (kulia) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania Young Scientists Tanzania (YST
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania Young Scientists Tanzania (YST) Dkt. Gozibert Kamugisha (kushoto) akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland baada ya kuwasili katika ukumbi wa  
Hoteli ya Golden Tulip Leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...