Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa kumekuwa na ukosefu wa maji kutokana na changamoto ya umeme iliyojitokeza kuanzia asubuhi ya tarehe 27.09.2022.

Hitilafu hiyo imesababisha mtambo kutoweza kufanya kazi   hivyo kupelekea upungufu wa huduma ya maji katika mji wa Bagamoyo na sehemu kubwa ya mkoa wa Dar es salaam.

Maeneo yanayoathirika ni pamoja na;
Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Kunduchi, Mbezi Beach, Goba, Mivumoni, Madale,  Kawe,  Lugalo, Makongo,  Chuo Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay,  Masaki,  Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti,  Ilala na Katikati ya mji.

Mafundi wa TANESCO wanaendelea na jitihada kuhakikisha huduma ya umeme inarejea.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202-121(WhatsApp tu)

Tovuti: www.dawasa.go.tz

Mitandao ya kijamii.

Facebook: https://www.facebook.com/pg/Dawasaofficial/posts/

Instagram: https://instagram.com/dawasatz?utm_medium=copy_link

Twitter: https://twitter.com/dawasatz?s=08

YouTube: https://youtube.com/channel/UCCVyHKIvUwDFG1tUyWhd7fQ

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...