Jengo la Masjala lililojengwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania lililozinduliwa na Alex Ngailo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Makete katika Kijiji cha Mwakauta Septemba 25, 2022.

Hafla ya uzinduzi huo ulishuhudiwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt Seraphia Mugembe, Mbunge wa Makete, Festo Sanga pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wananchi wa kijiji hicho.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Alex Ngailo na Mbunge wa Makete, Festo Sanga (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt Seraphia Mugembe pamoja na Mwenyekiti wa kijiji hicho, wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa  wa jengo hilo.
Mhandisi wa Ujenzi wa MKURABITA, Juma Mtali akimuonesha  Dkt Mugembe na viongozi wengine moja ya ofisi katika jengo hilo la Masjala ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya sh. mil. 46.
Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt Seraphia Mugembe, akihutubia katika hafla hiyo na kuahidi kununua samani kwa ajili ya ofisi hiyo pamoja na kugharamia uunganishaji umeme katika jengo hilo.
Mwakilishi wa DC Makete akihutubia wakati wa hafla hiyo. 

Mbunge wa Makete, Sanga akiwasalimia wananchi.
Dkt Mugembe akisalimiana na mmoja wa akina mama wa kijiji hicho.

Viongozi mbalimbali wakiungana kucheza wimbo wa dini wakati wa hafla hiyo..
Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Edward Mwaigombe aliyemwakilisha Mkurugenziu wa Halmashauri hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwakauta, Nelson Tweve akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo.


Ofisa wa Benki ya NMB akijitambulisha

Mhandisi wa Ujenzi wa MKURABITA, Juma Mtali akimuonesha  Dkt Mugembe na viongozi wengine moja ya ofisi katika jengo hilo la Masjala ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya sh. mil. 46.

Meneja Urasimishaji Mijini wa MKURABITA, Mwesiga Ileta  akijitambulisha.


Jengo la Masjala jipya na la zamani.

Bibi mkazi wa Kijiji cha Mwakauta akiwa na furaha baada jengo hilo kuzinduliwa.



Muonekano wa jengo hilo.

Choo kilichojengwa sambamba na jengo hilo


PICHA ZOTE NA RICHARD

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...