Na Vero Ignatus,Arusha.


Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)Kanda ya Kaskazini Katika kipindi cha julai 2021-juni 2022 ,ilisimamia uteketezaji wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitenganishi visivyofaa kwa matumizi yenye uzito watani 35.37 vyenye thamani ya tsh 2,007,981,981.54 , kati ya bidhaa hizo tani 6.83 zilikamatwa katika kaguzi mbalimbali, tani 28.54 wamiliki wake walizitolea taarifa huku jumla ya za hati za uteketezaji 60, ( dawa 36 na vifaa tiba 24) , na Ofisi ya Kanda ya Kaskazini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Adam Fimbo , wakati akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii septemba 2022, kwamba jumla ya maeneo 2167 yalikagulia,Smaeneo 1589 sawa na asilimia 73.3%yalikidhi matakwa ya kisheria ya dawa na vifaa tiba sura 219, majengo ambayo hayakukidhi viwango yalipewa maelekezo ya kufanya marekebisho ya upungufu uliobainika.

'' Changamoto kubwa tuliyonayo ni dawa kuingizwa kwa dawa bandia kupitia njia za panya ambazo hazijassajiliwa ila TMDA kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunadhibiti kwa kiasi kikubwa,kwani kwa sasa tunao wahudumu wachache na baadhi yao wanafanya kazi kwa mikataba mifupi,tumewaomba wabunge watusaidie ili wapate ajira ya kudumu'' alisema Fimbo

Sambamba na hayo alisema kuwa ufuatiliaji wa karibu wa chanjo ya Uviko19 aina ya Janssen jumla ya wateja 6512 ( wanaume 3,488 na wanawake 3,024) walifuatiliwa katika hudhurio la sita kwa kupigiwa simu na kujaziwa fomu maalum ya kutolea taarifa za usalama wa chanjo hiyo ambapo kati ya wateja wote waliofuatiliwa, wateja 884 walipata maudhi madogo na kupona na wateja 6 walipata madhara makubwa na kufariki.

Akizungumza mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo amesema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na anamna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi kwani wanatumia teknolojia ya kisasa ikiwemo mahabara ndogo ya kanda,na hiyo ya Namanga ambazo zinasaidia kutambua ubora wa wad awa na pale wanapotilia mashaka wanfanya mawasiliano na mahabara ya kanda Arusha na mahabara kuu iiyopo Dar es salaam

‘’Kiukweli tumeridhishwa na jinsi wizara inavyofanya kazi pamoja na mamlaka hii,sisi kwa niaba ya kamati ya bunge naeendelea kusisistiza kwamba waendelee kufanya kazi kwa nguvu kwasababu kazi yao ni ya kuhakikisha mipaka inakuwa salama kwa matumizi ya kibinadamu .

Kwa upande wake Naibu wa Waziri Wizara ya Afya Dkt.Godwin Mollel amewasisitiza watendaji katika mpaka huo wa Namanga kuhakikisha kuwa wanawapima watuwote wanaoingia na kutoka kwaajili ya Covid 19 pamoja na Ebola na kuwafuatilia kwa karibu zaidi huko wanapokwenda

''Hakikisheni anayeingia anaingia akiwa salama ili asiwapelekee tatizo watanzania,lakini vilevile wale wanaotoka watoke wakiwa salama asiwapelekee wengine waliopo upande wa pili matatizo''alisema Dkt.Mollel

Dkt.Mollel kuwa hiyo ni ziara ya kawaida ya kikazi ya Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii ,kutembelea kuangalia shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na wizara ya Afya pamoja na Taasisi zilizopo chini yake,imeona kazi zote zinazofanyika,hivyo kwa ujumla wao wametoa pongezi kwa Mkurugenzi mkuu wa TMDA kwani kwa maeneo yote waliyoyatembelea wameona kazi kubwa imefanyika

''Sisi kama wizara ya Afya kamati hii wametuomba tumsaidie Mkurugenzi mkuukwenye eneo zima la kupatikana kwa watendaji wakusaidia kufanya shughuli ziende kwa haraka,Kwani katika mpaka huu siyo shughuli zinazohusu wizara ya Afya pekee bali zinazohusu wizara zote ambazo zipo nchini zinazofuatilia kwaajili ya kusimamia mpaka wetu,,alisema Dkt.Mollel

Aidha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii wametembelea mkoa wa Arusha na kuangalia kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Dawa na Vitendanishi (TDMA)mpakani Namanga na wamejiridhisha na kuangalia utaratibu uliowekwa katika kudhibiti uingiaji wa dawa ambazo hazijasajiliwa na zile zinazopita ni zile zinazostahili

Naibu waziri wa Afya Godwin Mollel walipotembelea lipotembelea mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba TMDA kanda ya Kaskazini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa call na Vifaa tiba (TMDA) Adam Fimbo akiwasilisha taarifa fupi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya Jamii.

Baadhi ya Wafanyakazi katika Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA)
Kutoka katikati ni Kaimu meneja wa TMDA kanda ya Kaskazini Proches Patrick akiwa na watendaji wengine wa TMDA kutoka makao makuu.
Katika picha ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo walipotembelea Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela (hayupo pichani )
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya Jamii kutoka Zanzibar akichagia jambo
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya Jamii kutoka Zanzibar akichagia jambo

Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini Proches Patrick akionyesha Baadhi ya dawa zilizokamatwa zikiwa hazijasajiliwa na kutambuliwa ubora wake ,kushoto kwake ni mkaguzi wa dawa Kanda ya kaskazini Titus Malulu
Picha ya pamoja ya Kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya Jamii katika Mpaka wa Namanga walipokwenda kutembelea na kujionea utendaji kazi uanavyoendea




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...