Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba mapendekezo na maoni yaliyokusanywa na Kikosi Kazi maalum kuhusu Amani na Demokrasia ya Zanzibar, ni uwekezaji Mkubwa unaoweza kuisaidia Zanzibar katika kuendeleza amani ya kweli .

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipokutana na kupokea ripoti ya Kikosi Kazi Maalum cha kinachokusanya maoni ya Wadau juu ya ujenzi wa marididhiano na Amani Zanzibar kinachoundwa na kujumuisha wadau mbali mbali wa Demokrasia, Dini na Asasi za Kiraia.

Amesema kwamba hapa Zanzibar kwa muda mrefu imeonekana kwamba maridhiano ni ya wanasiasa pekee na kwamba kuwepo kwa jitihada hizo ni jambo muhimu litakalosaidia kuweka mustakabali bora wa Zanzibar.

Mhe. Othman amesema kwamba jambo hilo linatoa nafasi kwa wananchi na wadau kutoa maoni yao juu ya kile wanachokitaka katika nchi na ni busara kwa serikali ichukue na kutekeleza matakwa ya wananchi juu ya mtazamo sahihi unaohusu mustakabali wa nchi yao.

Aidha Mhe. Makamu amefahamisha kwamba kuwepo maoni hayo ni fursa muhimu ya kuendeleza Demokrasia na Amani ya kweli katika kuendeleza maridhiano na serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini kuwa endelevu.

Amesema kwamba utekelezaji wa maoni hayo unahitaji sana wanasiasa na viongozi kubadili fikra na mtazamo wao juu ya masuala mbali mbali yanayoihusu nchi katika kujenga mustakabali bora na kujenga Zanzibar yenye Amani na maendeleo.

Hata hivyo , Mhe. Othman ameshauri kwamba ni vyema kwa wanasiasa kuondosha zana mbaya kwa kwenye kuangalia mfumo wa masuala mbali mbali kwenye ujezi wa Demokrasia zikiwemo taratibu na sheria za uchaguzi katika mtazamo wa kimageuzi ya kidemokrasia.

Aidha amesema kwamba viongozi na wanasiasa pamoja wananchi na wadau wengine ndio msingi muhimu wa kusaidia kujenga khatma njema ya Zanzibar katika kuyaendea masuala mbali mbali yanayohusu nchi yao.

Mapema Katibu wa Kikosi Kazi hicho Suleiman Bajuni, ameeleza kwamba Kikosi hicho kimefanya kazi ya kukutana na wadau mbali mbali na kupata maoni na mependekezo yao muhimu ya awali juu ya kuimarisha Demokrasia, amani kabla, wakati na baada ya Uchaguzi nchini.

Amesema kwamba juhudi kubwa juhudi hiyo inalenga pia katika kupatika maridhiano endelevu yanayojumuisha matakwa ya wananchi na kukubalika na wadau mbali mbali na hivyo kuchangia ustawi bora wa maendeleo ya nchi kidemokrasia.

Ameongeza kuwa baada ya rasimu hiyo ya maoni imenonekana kwamba kuna haja kubwa ya kuwepo mabadiliko katika maeneo mbali mbali hasa ya nayohusu sheria na taratibu za uchaguzi katika kuchangia kujenga uzalendo ndani ya Zanzibar.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akimsikiliza Kaimu M/Kiti wa kikosi kazi kinachokusanya maoni ya wadau juu ya ujenzi wa maridhiano na amani Zanzibar. Kikosi hicho kimefika ofisini Kwa makamu kuwasilisha ripoti ya maoni ya wadau Leo tarehe 29.9.22 picha na ofisi ya Makamu kitengo cha Habari




Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akizungumza na kikosi kazi kinachokusanya maoni ya wadau juu ya ujenzi wa maridhiano na amani Zanzibar. Kikosi hicho kimefika ofisini Kwa makamu kuwasilisha ripoti ya maoni ya wadau Leo tarehe 29.9.22 picha na ofisi ya Makamu kitengo cha Habari



Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, (watu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja kikosi kazi kinachokusanya maoni ya wadau juu ya ujenzi wa maridhiano na amani Zanzibar. Kikosi hicho kimefika ofisini Kwa makamu kuwasilisha ripoti ya maoni ya wadau Leo tarehe 29.9.22 picha na ofisi ya Makamu kitengo cha Habari







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...