Na.Khadija Seif, Mtwara 

BONDIA wa Ngumi za kulipwa Karim Mandonga ametamba kumchezesha mpinzani wake Baikoko , Salim Abeid katika uwanja wa Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara septemba 24 mwaka huu kuelekea pambano la "Ubabe Ubabe 2" kati ya Twaha Kiduku dhidi ya mpinzani wake Abdo Khaled kutoka Misri.

Akizungumza mara baada ya kupima Afya na kumaliza maandalizi ya mwisho  kabla ya kupanda ulingoni kwa Mabondia mbalimbali katika stendi ya zamani Mkoani Mtwara, Bondia wa Kitaifa Twaha Kassim "Kiduku" amesema amejiandaa vizuri kupanda ulingoni dhidi ya mpinzani wake Abdo Khaled kutoka Misri pambano la uzani wa super Middle raundi 10 Huku Kiduku akihaidi kuwapa ushindi watanzania  mapema tu na kunyakua mkanda wa UBO.

Hata hivyo nae Bondia kutoka Morogoro mwenye tambo na kipenzi cha watanzania kwa sasa  Mandonga "Mtu kazi" ameendeleza tambo zake kuwa yuko tayari kumchezesha mpinzani wake Baikoko mbele ya ulingo na watanzania wasubiri Mandonga akifanya maajabu yake.

Mabondia Wengine watakao panda Ulingoni usiku wa kesho Fransic Miyeyusho dhidi ya Adam Lazaro, Karim mandonga mtu kazi na Salim Abeid, Nasra Msami na Halima Bandora,Osama Arabi wa mtwara na Emilian Polino kutoka JKT huku Pambano kuu Twaha kiduku na Abdo Khaled kwa raundi 10 Katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.


Bondia kutoka nchini Tanzania Twaha Kiduku dhidi ya mpinzani wake kutoka Misri Abdo Khaled wakiwa na mkanda wa UBO ambao katika uwanja wa Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara septemba 24 watapambania mkanda huo

Bondia Halima Bandola akiwa na mpinzani wake Nasra Msami wakifanya zoezi la kutazamana (face_off) mara baada ya kumaliza zoezi la upimaji wa Afya na uzito lililofanyika  mapema Leo septemba 24 katika stendi ya zamani Mkoani MtwaraMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...