Mashindano ya Mungai Memorial cup yanatarajia kutimua vumbi jumamosi tarehe 31 septemba katika viwanja vya Wenda yenye lengo la kumkumbuka mzee Joseph Mungai pamoja na kudumisha umoja

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya mufindi Mh Saad Mtambule amesema mashindano hayo yanaenda kuongeza ushirikiano kwa vijana pamoja na kujiepusha na vitendo vya ukatili.

Aidha Mtambule amebainisha kuwa kupitia mashindano hayo ya Mungai memorial cup yanaenda kurejesha heshima ya soka katika wilaya ya mufindi iliyofifia kwa miaka ya hivi karibuni

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mufindi Gift Mwachan'ga amesema wamejipanga vyema kuendesha mashindano hayo yatakayowakutanisha timu mbalimbali pamoja na kuibua vipaji

Miongoni mwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo ni misitu fc pamoja na bajaji fc kwa upande wao wamejinasibu kufanya vyema katika mashindano hayo na kutwaa kikombe hicho

Mashindano hayo yatashirikisha takribani timu nane kutoka wilaya ya mufindi huku mtindo utakaotumika ni mtoano mpaka kufikia hatua ya fainali mnamo tarehe 13 ya mwezi wa kumi 2022.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...