Na Mwandishi wetu, Simanjiro

MGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara, Anna Moinan Shinini amesema endapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo atahakikisha anaondoa makundi na mgawanyiko uliopo Simanjiro.

Juzi Halmashauri kuu ya CCM Taifa ilirudisha majina matatu ya Anna Shinini, Kiria Laizer na Haiyo Mamasita, kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro.

Shinini amesema endapo wajumbe watamchagua kushika nafasi hiyo, watarajie maendeleo makubwa na umoja, kwani makundi na mgawanyiko uliopo hivi sasa unazorotesha maendeleo.

"Hivi sasa kuna mgawanyiko mkubwa sana Simanjiro nataka niwaunganishe wana Simanjiro wawe wamoja na kuachana na mgawanyiko na makundi ya kisiasa," amesema Anna.

Hata hivyo, ameishukuru Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumpa heshima ya kugombea nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa CCM na kurudisha jina lake.

"Nakushukuru chama changu kwa kunipa ridhaa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro, ni heshima kubwa mno wamenipa," amesema Anna.

Kabla ya kupata fursa hiyo Anna aligombea na kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa CCM (UWT) kwa kupata kura 97.

"Hata hivyo ikabidi uchaguzi urudiwe japo sikuridhika nimekata rufaa kwani nilishinda awali na uliporudiwa baadhi ya wajumbe waliondoka kabla ya kupiga kura na baadhi ya wanasiasa walicheza mchezo mchafu," amesema Anna.

Katibu wa UWT Wilaya ya Simanjiro Leokadia Fisoo amesema Anna alipata kura 97, Agnes Brown Ole Suya 86, Naomi Edward 10 na Rehema Yohana 2.

"Hata hivyo uchaguzi ikabidi urudiwe kutokana na Anna kutopata zaidi ya nusu ya kura na ziliporudiwa Agnes akapata kura 99 na Anna kura 96," amesema Fissoo.

Mkazi wa Kijiji cha Loiborsoit Kata ya Emboreet, Loti Mollel amesema Anna ni kiongozi mzuri na mfano wa kuigwa kwani amefanikisha maendeleo mbalimbali kwenye eneo hilo.

"Ameacha alama kubwa ya maendeleo kwani kwa kutumia shilingi milioni 200 amechimba visima vitatu vya maji na kuwezesha wanawake kupitia miradi ya mboga mboga," amesema Mollel.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...