Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint) ili kuvutia uwekezaji na kuwezesha ufanyaji biashara wenye tija utaokuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia Ukuzaji wa Uchumi na Taasisi kutoka Benki ya Dunia (WB), Dr.Asad Alam na ujumbe wake kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma Septemba 29, 2022.

Akiwa ameambata na Viongozi wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara akiwemo Naibu Katibu Mkuu Dkt. Hashil Abdallah, Dkt. Kijaji amemhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha na kuendeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wajasikiamaki wadogo na wa kati kuwekeza na kufanya biashara ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea kufanya mamoresho mbalimbali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini ( Blueprint) ikiwemo kupitia na kurekebisha sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uwekezaji pamoja na kupunguza tozo mbalimba ambazo zimekuwa kikwazo katika ufanyaji biashara na uwekwzaji.

Naye Mkurugenzi huyo wa Kikanda chini ya Benki ya Dunia amesema Programu hiyo ya kukuza uchumi na Taasisi amesema Benki dunia kupiyia programu hiyo iko tayali kuwawezesha wajasilimali watanzania katika sekta mbalimbali kuendeleza biashara zao zitakazoongeza ajira, pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi kwa ujumla.






 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...