WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango mkubwa uliotolewa na marehemu Balozi Paul Rupia wakati wa utumishi wake na hata baada ya kustaafu.

“Moja ya jambo ambalo halitasahaulika ni uthubitu wake wa kuanzisha Benki ya Watu wa Dar es Salaam (DCB) ambayo alikuwa mwenyekiti wake na hadi anaondoka katika uongozi aliicha benki hiyo ikiwa na matawi manane na moja kati ya hayo likiwa jijini Dodoma.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema hayo leo Ijumaa (Septemba 23, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuuaga mwili wa marehemu Balozi Paul Rupia, katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Rais Samia amenituma kuja kumuwakilisha katika msiba huu, amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Balozi Rupia, hakuweza kuhudhuria kwa sababu yupo nchini Msumbiji kwa ziara ya kikazi. Pia ametoa pole kwa familia na waombolezaji wote.”

Mheshimiwa Majaliwa amewasihi Watanzania kumuombea marehemu na familia yake kwa Mwenyezi Mungu ili apate pumziko la milele na familia iwe na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba amesema marehemu Balozi Rupia alichangia kwa kiasi kikubwa mageuzi ya uchumi nchini na kuanzisha mageuzi ya kisiasa ya mfumo wa vyama vingi nchini.

Awali, Mwenyekiti wa Mabalozi Wastaafu wa Tanzania, Balozi James Msekela amesema marehemu Balozi Rupia atadumu katika historia ya Tanzania kama mwanasiasa mahiri na mwanadiplomasia nguli.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa marehemu Balozi Paul Rupia, katika viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2022 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia, katika viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2022 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa marehemu Balozi Paul Rupia, katika viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2022 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...