Serikali imeendelea kuvitangaza na kuviendeleza vivutio mbalimbali vya utalii kwa kushirikiana na wadau wa utalii nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu maswali kuhusu uendelezaji wa vivutio vya utalii vya Wilayani Ukerewe na uboreshaji wa Hifadhi ya Taifa Kitulo Bungeni jijini Dodoma leo.

Amesema katika Kisiwa cha Ukerewe Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Maafisa wa Mkoa wa Mwanza walitekeleza zoezi la kubaini na kuvitambua vivutio vya utalii vilivyopo katika kisiwa hicho.

“Vivutio vilivyotambuliwa ni pamoja na utalii wa ikolojia, utalii wa fukwe, utalii wa kiutamaduni na kihistoria” Mhe. Masanja amefafanua. 

Amesema ili kuboresha utalii wa ĂȘneo hilo Serikali inaendelea kuimarisha Ofisi ya Kanda ya Utalii iliyopo Jijini Mwanza na kuanzisha Chuo cha Utalii cha Taifa katika Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kusogeza huduma Kanda ya Ziwa.

Aidha, amesema Wizara imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara ndani ya Hifadhi ya Taifa Kitulo, kuanzisha huduma za malazi na chakula, kuongeza mazao mapya ya utalii kama vile utalii wa kutumia baiskeli, utalii wa kutembea kwa miguu na utalii wa kupanda vilima.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo ndani ya Hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya watalii na idadi ya siku za kukaa hifadhini na hivyo kuongeza mapato.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...