Na Jane Edward,Arusha.


Wanafunzi wanaosoma kozi za udaktari katika vyuo mbalimbali wametakiwa kujikita katika kusomea fani ya madaktari bingwa wa upasuaji wa maradhi ya njia ya mkojo na uzazi kutokana na uhaba wa madaktari hao kwani waliopo hivi sasa ni 100 tu .

Hayo yalisemwa jijini Arusha na Rais wa chama cha Madaktari bingwa wa upasuaji wa maradhi ya njia ya mkojo na uzazi (TAUS),Prof .Chalonde Yongolo wakati akizungumza kwenye kongamano la kisayansi pamoja na mkutano mkuu wa TAUS unaofanyika jijini Arusha.

Profesa Yongolo amesema kuwa,idadi ya madaktari bingwa katika sekta hiyo bado ni changamoto ambapo kwa idadi hiyo ya madaktari 100 ni sawa na daktari 1 kuhudumia wagonjwa laki 6.

Ameongeza kuwa, wanataka kuhakikisha wanakuwa na mikakati wa kuwa na madaktari bingwa katika kila wilaya ili kuziba pengo hilo .

Naye Katibu mkuu wa TAUS ,Dokta Deogratius Mahenda amesema kuwa, watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea ndio wanakabiliwa na changamoto ya matatizo ya mfumo wa mkojo na uzazi na hiyo ni kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya kutosha na kuweza kuwahi kwa wataalamu kabla ya tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.

Naye Daktari bingwa wa upasuaji katika mfumo wa mkojo , uzazi kwa wanaume na upandikizaji wa figo,Dk Victor Sensa amesema kuwa , wamejipanga kuhakikisha wanahamasisha vijana wengi waliopo vyuoni wanajiunga na fani hiyo,huku wakiiomba serikali iwanunulie vifaa kwani viliyopo ni vichache havitoshi ,hivyo iongeze nguvu kwenye ununuzi wa vifaa katika fani hiyo.

Awali akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema ni wakati wa madaktari hao kutoa elimu zaidi kwenye maradhi ya njia ya mkojo kutokana na udanganyifu wa tiba za njia ya mkojo uliopo mitaani hivi sasa.

Amesema maradhi ya mkojo yamekuwa tishio kubwa kwa nguvu kazi hususani vijana kutokana na hali ya mtindo wa maisha pamoja na kudanganyana hali inayoibua maradhi mengine na kupoteza nguvu kazi hiyo ambao ndiyo baba wa Taifa hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akipokea zawadi kutoka kwa waoneshaji mabanda katika kongamano hilo.
Mongela akizungumza na wadau wa mkutano huo.
Rais wa TAUS Prof,Cholonde Yongolo akizungumza na waandishi wa Habari jijini Arusha.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...