Na Mwamvua Mwinyi,Kwala
WIZARA
ya Maji imebariki kibali cha matumizi ya sh.bilioni 20 zitazopeleka
maji katika eneo la Kwala, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa
Pwani.
Ridhiki Shemdoe
ambae ni Katibu Mkuu TAMISEMI, aliyasema katika ziara Maalumu ya kukagua
kazi zinazoendelea za kukamilisha Mradi huo.
"Wizara
ya Maji tayari imeshatoa kibari cha matumizi ya fedha kiasi cha
shilingi bilioni 20, zitazopeleka maji kwenye Jiji la Kibiashara la
Kwala, lengo kuhakikisha Mradi huo unakuwa na miundombinu yote,"
alieleza Shemdoe.
Kwa
upande Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi John
Kijazi alipongeza kuhudi za ujenzi wa Jiji hilo, huku akiwataka
wataalamu kutoka Wizara hizo kujiongeza katika kubiresha Jiji badala ya
kufungwa na yaliyokuwa kwenye makabradha.
Gabriel Joseph Katibu Mkuu Uchukuzi aliuhakikishia msafara huo kwamba Mradi, utakamilika kama ilivyopangwa.
"Magari
yote yatayoleta makontena hapa nchini yataishia hapa Kwala,
yanayokwenda nchi za nje pia yatachukuliwa hapa, yakitokea Dar es Salaam
yakiletwa kwa Treni," alisema Gabriel.
Ally
Gugu Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
alipongeza Serikali kwa Uwekezaji huo, unaolenga kupunguza msongamano
katika Jiji la Dar es Salaam.
Mhandisi
Telchemis Mramba aliwapongeza wataalamu kutoka Wizara hizo, ambao
wamepiga kambi Kwala kufanikisha kukamilika kwa Mradi huo.
"Niwapongeze
Wataalamu wetu kwa kazi mnayoendelea kuitekeleza hapa Kwala, tunataraji
zoezi ili litakamilika kama ilivyopangwa na Serikali yetu chini ya Rais
Samia Suluhu," alisema Mramba.
Awali
mmoja wa Wataalamu kutoka TAMISEMI Miringay Joseph, aliwaelezea
makatibu hao namna kazi zinavyokwenda, huku wakieleza kwamba itakamilika
kama ilivyopangwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...