Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv

Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022, zimefika salama Mkoani Kagera, mapema leo Oktoba 06, 2022 ukiwa ni Mkoa wa Mwisho kwa kabla ya kuhitimishwa Kilele cha Mbio hizo mnamo Oktoba 14 ambapo ukiwa Mkoani Kagera unaatarajia kukagua, kutembelea na kuzindua jumla ya miradi 37 ya Afya, Elimu, Maji, Barabara na miradi ya watu binafsi kwa Halmashauri nane yenye thamani ya Tsh. bilioni 13.6.

Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Biharamulo ukitokea Mkoani Kigoma, na kuzindua mradi wa Maji Ruganzu, vyumba 2 vya madarasa Shule ya Wasichana Kagongo kwa fedha za UVIKO-19.

Miradi miwili imewekewa Jiwe la msingi ambayo ni Mradi wa barabara ya Lami, Rukaragata-Kibamba yenye urefu wa km 1 na Kituo cha Afya cha Bisibo kwa fedha za Tozo, Sambamba na kukagua shughuli za Lishe, mapambano dhidi ya Malaria, Mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kuzindua klabu ya Wapinga Rushwa shule ya Sekondari Nyakanazi.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua mradi wa maji Ruganzu, uliopo Kata ya Nyanza, Wilaya ya Biharamulo wenye thamani ya Tsh. milion 114.3 uliojengwa na Shirika la Community Based Health Care Council (CBHCC) na nguvu za jamii, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022, Ndg. Sahili Geraruma amewasihi wananchi hao baada ya mradi kukamilika ni vema sasa wananchi waunganishe huduma ya maji katika makazi yao ili kukamilisha dhana ya kumtua mama ndoo kichwani.

“Ili kuunga juhudi za Mhe. Samia za kumtua mama ndoo kichwani yatupasa kuunganisha huduma ya Maji katika nyumba zetu, lakini kumuacha mama aendelee kufuata maji mita mia mbili au mita mia tatu tunakuwa bado hatujatimiza lengo la kumtua mama ndoo kichwani, hivyo nawasihi wananchi tuhakikishe kila mmoja wetu anaunganisha huduma ya maji katika makazi yake,”ameeleza Geraruma.

Sambamba na hilo amewashukuru wahisani CBHCC kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango na kuwasihi maeneo yote yaliyojengwa vituo vya kuchotea maji yawekewe uzio ili kuzuia hujuma kwenye miundombinu na mradi uendelee kuwa endelevu.

Aidha, amewataka watalaam wanaosimamia miradi ya Serikali kuhakikisha wanafuata taratibu na maelekezo ya matumizi ya fedha kama vile miongozo inavyowaelekeza ili miradi iwe yenye tija na yenye manufaa kwa wananchi.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Ndg. Geraruma akizindua Mradi wa Maji Ruganzu Wilayani Biharamulo
Barabara ya Rukaragata Wilayani Biharamulo iliyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Yenye urefu wa Kilometa Moja
 Wakuu wa Mikoa ya Kagera na Kigoma Wakikabidhiana Mwenge wa Uhuru 2022 katika Eneo la Makabidhiano Katika Kata ya Kalenge Wilayani Biharamulo

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Ndg. Sahil Nyanzabara Geraruma Akiongea na Wanaklabu ya Wapinga Rushwa wa Shule ya Sekondari Nyakanazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...