Msajili wa Hazina Benedicto Mgonya akizungumza wakati uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza na mafanikio ya NIC wakati uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa Mteja uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Msajili wa Hazina Benedicto Mgonya akiwa na baadhi ya wa NIC pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi mgeni mwalikwa wakionesha bango la ahadi kwa mteja mara baada ya kuzinduliwa kwa mkataba wa huduma kwa mteja.
Mgeni Rasmi Msajili wa Hazina Benedicto Mgonya akiwa katika picha ya  pamoja na Menejimenti ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) mara baada ya kuzinduliwa kwa Mkataba wa Huduma kwa Mteja , jijini Dar es Salaam.

*Yaahidi kwenda kwenda kufungua ukurasa mpya wa mafanikio ya huduma bora kwa wateja

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) imezindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja ukiwa na lengo ya kutoa huduma bora kwa wateja na zenye viwango.

Akizungumza wakati uzinduzi wa Mkataba huo, Msajili wa Hazina Mgonya Benedicto amewataka watumishi wa NIC kufuata ahadi iliyowekwa kwenye mkataba huo na asiwepo mtumishi yeyote wa kutenda kinyume na mkataba huo kwani atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

Amesema madhumuni ya mkataba huu ni kuboresha uhusiano baina ya Shirika na wateja wake lakini pia ukikusudia kuongeza uelewa kuhusu aina na ubora wa huduma zinazotolewa, haki na wajibu wa mteja na jinsi anavyoweza kuwasiliana.

"Mkataba wa Huduma kwa Mteja ni makubaliano kati yenu watoa huduma na mteja wenu ikiwa ni ahadi ya kutoa huduma bora kwa mteja, mkataba huu unaelekeza na kuainisha viwango vya huduma ambavyo wateja wenu wanatarajia kupata ili kufikia malengo yao". Amesema

Aidha amesema Ofisi ya Msajili wa Hazina na Serikali kwa ujumla ipo tayari kuwapa ushirikiano mnaostahili ikiwa tu mtaweka bidii katika kazi na kuboresha huduma zaidi ya zilivyo sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Elirehema Doriye, amesema Shirika limekuwa likifanya mabadilikko kwenye kuwahudumia wateja ambapo wamekuwa wakiboresha huduma ili kuendana na ushindani ulioko sokoni jambo lililowavutia wateja kununua bidhaa zao za Bima na kuwafanya kuwa na ukuaji wa faida ya zaidi ya asilimia 100 katika miaka minne mfululizo.

"Mojawapo ya misingi inayotuongoza NIC yetu ni kutambua kuwa siku zote "Mteja Kwanza" yaani "Customer first" hii inamaanisha kwamba mteja kwetu ni kipaumbele namba moja katika utoaji huduma". Amesema Dkt.Doriye.

Aidha Dkt.Doriye amesema katika kuadhimisha wiki hii na kutambua umuhimu wa wateja, Shirika limezindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja "ikiwa ni ahadi yetu kwa wateja kuwa tutawapatia huduma inayostahili kulingana na ahadi tuliyowapa". Amesema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...