Na Mwandishi Wetu,MEXICO

TANZANIA imeshirki katika Kongamano la Dunia la Sera za Utamaduni na Maendeleo Endelevu la UNESCO - MONDIACULT 2022, ambalo limefanyika limefanyika kuanzia Septemba 28 hadi 30, 2022 Mexico.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa ametuma ujumbe waTanzania katika Kongamano hilo la Mawaziri wa Utamaduni wa nchi wanachama wa UNESCO kupitia Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samweli Shelukindo ambaye aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya utamaduni Dkt. Julieth Kabyemela.

Akiwasilisha ujumbe huo, Balozi Shelukindo amesema katika kuendeleza na kulinda utamaduni ipo haja ya kulinda maeneo ya kitamaduni, kulinda aina zote za urithi wa kitamaduni, kulinda na kusaidia wataalamu wa kitamaduni, kukuza ubunifu, uvumbuzi, na kuunganisha sekta ya sanaa na utamaduni katika mipango yote ya maendeleo.

"Ni ukweli usiopingika kwamba kutumia historia na utamaduni wa kipekee wa kila jumuiya, kunaweza kutoa masuluhisho ya kudumu ambayo yanaathiri jamii zetu kiuchumi na kijamii” Lakini pia alisema pamoja na umuhimu wa uridhi wa kiutamaduni ”alisema Balozi Shelukindo.

Kongamano hilo lililokuwa na lengo la kujadili sera za Utamaduni na vipaumbele vyake ili ziweze kujikita kikamilifu katika mitazamo ya maendeleo endelevu pamoja na kukuza mshikamano, amani na usalama, kulingana na dira ya UNESCO ya mwaka 2021,ambapo Tanzania ina imani kuwa matokeo ya kongamano hilo la MONDIACULT 2022, yatakuwa ni hatua kubwa katika juhudi za kuandaa sera bora za kitamaduni.

Mhe. Balozi Samwel William Shelukindo, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Shirika la Elimu, Sayansi na Technolojia (UNESCO) akizungumza katika mkutano huo
Mhe. Samwel W. Shelukindo, wa pili kutoka kulia akishiriki katika jopo la kujadili sera za utamaduni na maendeleo endelevu la MONDIACULT nchini Mexico


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...