Mkurugenzi wa uratibu wa udahili na manajimenti ya data, Dkt. Kokuberwa Mollel akizungumza na waandishi wa habari akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la nne la udahili kwa mwaka wa masomo 2022/2023 leo Oktoba 3, 2022 jijini Dar es Salaam

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
TUME ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imefungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne kwa mwaka wa masomo 2022/2023 dirisha ambalo litaanza leo Oktoba 3 hadi Oktoba 24 mwaka huu 2022.

Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa udahili wa awamu tatu na kuonekana kuna baadhi ya wanafunzi hawakuweza kukamilisha ufadhili wao katika dirisha la kwanza hadi la tatu ukizingatia wakati huu ambao Taasisi za Elimu ya juu nchini zinasema kuwa kuna nafasi katika baadhi ya masomo kwa mwaka huu wa masomo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 3, 2022 Mkurugenzi wa uratibu wa udahili na Manajimenti ya data Dkt. Kokuberwa Mollel amesema lengo la kufungua dirisha la tatu ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali.

Jumla ya wanafunzi 172,868 walitarajiwa kudahiliwa lakini mpaka sasa wanafunzi 110068 ndio amekwisha kudahiliwa na nafasi 62,150 ndizo zimebakia.

"Tume imepokea maombi ya kuongezea muda wa udahili kutoka kwa baadhi ya wa waombaji na ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi katika baadhi ya Programu za masomo kwa mwaka 2022/2023.

Aidha tume imevitaka vyuo kuhakikisha Program ambazo watafungua katika dirisha hili ni zile zenye nafasi tu huku zile ambazo zimejaa wakitakiwa kuendelea Kuzifunga ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza Kujitokeza hapo baadae.

Pia imewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahili ama kujithibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.

Dkt. Mollel amesema zoezi la uhakiki wanafunzi kwa wale ambao walidahiliwa kwenye chuo zaidi ya kimoja linaendelea ambapo linatarajiwa kukamilika Oktoba 24. 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...