·      Wanafunzi wote Hazina wapata alama A moko

 

Na Mwandishi Wetu

 SHULE ya Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam, imeendelea kutesa kwenye matokeo ya utahimilifu (moko) Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wanafunzi wote waliofanya mtihani huo wamepata alama A.

 Mkuu wa taaluma wa shule hiyo, Wilson Otieno alisema jana kwamba matokeo hayo mazuri yamewapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri hadi kwenye mtihani wa darasa la saba .

 Alisema matokeo hayo yameifanya kuwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya mtihani huo wa utahimilifu.

 Otieno alisema wastani wa shule nzima imepata alama 283/300 ambayo ni sawa na band 1 ikimaanisha kwamba ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo hayo ya mwaka huu.

 Alisema mwanafunzi wa kwanza kwenye shule hiyo ni Blessing Mayombo, ambaye amepata alama 293 kati ya 300 ya alama zote zinazotakiwa kwenye masomo yote.

 Alisema mbali na kufanya vizuri kwenye matokeo ya moko Mkoa, shule hiyo imekuwa ikiongoza kwa Wilaya ya Kinondoni kwa mwaka wa pili mfululizo.

 “Mwaka 2021 na mwaka huu tena shule ya Hazina imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam tunashukuru kwa mafanikio haya na tunaahidi kuwaandaa wanafunzi wetu waweze kufanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba,” alisema

 Alisema siri ya mafanikio hayo ni kujituma kwa walimu na ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata kwa uongozi wa shule na wanafunzi ndiyo kitu wanachojivunia.

 “Walimu wanafanyakazi kwa moyo sana, wazazi wa wanafunzi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri sana kwa shule na uongozi wa shule unawajali sana walimu, hayo kwa pamoja yamekuwa yakisaidia ufaulu wetu kuwa juu mwaka hadi mwaka,” alisema

 Aliwapongeza wanafunzi kwa mafanikio hayo na kuwataka wasome kwa bidii ili hatimaye waweze kuendelea kuongoza kitaifa na  Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mitihani ijayo.

 

Mkuu wa taaluma wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Wilson Otieno akimpa tuzo mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Blessing Mayongo jana  kwa kufanikiwa kuongoza kwenye matokeo ya shule hiyo ya mtihani wa utahimilifu (moko) kwa kupata alama 293 kati ya 300 zinazotakiwa .


Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni Dar es Salaam wakishangilia baada ya wote kupata alama A kwenye mtihani wa utahimilifu (moko) matokeo yaliyotoka hivi karibuni
Mkuu wa taaluma wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Wilson Otieno akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo baada ya wote kupata alama A kwenye matokeo ya mtihani wa utahimilifu mkoa wa Dar es Salaam
Wanafunzi walioingia 10 bora kwa shule ya Hazina matokeo ya mtihani wa utahimilifu Mkoa wa Dar es Saalam wakishangilia baada ya kupata matokeo yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...