Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza ufanyike upembuzi kawa mashauri yote ya ardhi yaliyokaa muda mrefu kutokana na sababu zisizo na mashiko.

Amemtaka Msajili wa Mabara ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo kusimamia agizo hilo kwa kumpatia taarifa mapema mwezi Novemba 2022.

Aidha, alimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuangalia kwa jicho la tatu Mabaraza yote ya Ardhi ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya mlundikanao wa kesi za muda mrefu.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo Oktoba 6, 2022 wakati wa Kikao kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt Mabula alisema, serikali inatambua umuhimu na michango ya mawakili katika kuvisaidia vyombo vya utoaji haki na kuwakumbusha mawakili suala la maadili ya kiutendaj hasa kwa baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, uzoefu unaonesha mashauri mengi yanayowakilishwa na mawakili ndiyo yenye kuchukua muda mrefu kumalizika.

‘’Mshauri mengi ya ardhi katika mabaraza hayapewi kipaumbele na Wakili anaweza kupanga tarehe ya kesi ambayo kwa siku hiyo ana mashauri katika vyombo vingine vya kutoa haki ‘’

Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha pia baadhi ya mapingamizi yana dhamira ya kupoteza muda hususan yale mashauri yanayohusu taasisi za fedha.

‘’Mashauri mengi yanayofunguliwa na wananchi walioshindwa kurejesha mikopo  kwa wakati au kukiuka mikataba ya mikopo, wananchi wanakimbilia kwenye mabaraza kwa kushauriwa na mawakili’’. Alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, ucheleweshaji mashauri kwa sababu zozote zile ni kuchelewesha kupata haki kwa wakati na kutoa rai kwa mawakili kuona umuhimu wa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutumia nafasi zao kama maafisa wa mahakama kwa nia ya kuhakikisha mashauri ya ardhi yanamalizika kwa wakati na kwa haki kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi alisema, wizara yake imeitisha kikao cha pamoja na mawakili wa kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha mashauri ya ardhi katika mabaraza yanasikilizwa na kumalizwa kwa wakati.

‘’Mawakili wa kujitegemea mnapotekeleza kwa uadilifu uaminifu na weledi jukumu lenu la kuwakilisha wananchi katika mashauri mnawarahisishia wenyeviti wa mabaraza ya ardhi kazi ya kusikiliza na kutoa maamuzi kwa wakati kwani uwakilishi wenu kwa namna moja ama nyingine unatoa dira mapema ya kufahamu mwananchi yupi ana haki na yupi hana haki katika shauri husika’’ alisema Dkt Kijazi.

Kikao Kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kina lengo la kupata uelewa wa pamoja, kupokea changamoto wanazokutana nazo katika mabarza ya ardhi pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na TLS katika kutatua kero za wananchi nwenye mashauri ya ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili Kulia) pamoja na Katibu Mkuu Dkt Allan Kijazi (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara wakiwasili kwenye kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wnasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifungua kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.

Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi baina ya Kitengo cha Mbaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza katika kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Abdi Kagomba (katikati) wakati wa kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba na Wilaya kilichofanyika  Oktoba 6, 2022 jijini DodomaKushoto ni Wakili Msomi Ally Nkangaa. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...