Na Mwandishi Wetu

SPIKA Mstaafu ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha  Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda anatarajiwa kuwatunuku wahitimu 291 wa masomo mbalimbali kwenye mahafali ya 20 ya Chuo hicho.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Yohana Mashalla, amesema leo kuwa mahafali hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 3 Desemba 2022 yatatanguliwa na Kusanyiko la Wahitimu (Convocation) siku ya Ijumaa tarehe 2 Desemba 2022 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Marekani nchini.

Alisema kauli mbiu ya kusanyiko hilo la wahitimu mwaka huu ni “kukuza ubunifu ili kuimarisha mifumo ya utoaji wa afya”  na kuongeza kuwa kwenye tukio hilo wanafunzi waliofanya vizuri (best students) katika mitihani yao watapewa zawadi mbalimbali.

Kuhusu Mahafali alisema, yatahudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Afya na Elimu Kairuki (KHEN), Kokushubira Kairuki na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha (HKMU) Bwana John Ulanga, viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali, wadau wa mendeleo na wageni waalikwa.

Alisema kwenye mahafali hayo kutakuwa na jumla ya wahitimu 291, kati yao wanawake ni 170 na wanaume ni 121.

Aliongeza kuwa wahitimu 54 watatunukiwa Stashahada ya Uuguzi, 10 Stashahada ya Ustawi wa Jamii, 38 Shahada ya Uuguzi. Wahitimu 177 watatunukiwa Shahada ya Udaktari wa Binadamu kati yao wanawake ni 97 na wanaume ni 80.

Profesa Mashalla aliongeza kusema kwenye mahafali hayo pia jumla ya wahitimu 12 watatunukiwa shahada za Uzamili, kati yao 10 watatunukiwa Shahada ya Uzamili ya Tiba na Afya ya Watoto (MMED, Peadiatrics and Child Health).

Alisema mwanaume mmoja atatunukiwa Shahada ya Uzamili ya Upasuaji (MMED, surgery) na mwanamke mmoja atatunukiwa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Afya ya Jamii (MSc, Public Health).

“Nawapongeza wahadhiri, maprofesa pamoja na watumishi wote wa HKMU kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya kuwalea na kuwafundisha wahitumu wote wanaotarajiwa kutunukiwa vyeti, stashahada na shahada siku ya Jumamosi,” alisema Profesa Mashalla.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Profesa Yohana Mashalla
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu  ya Afya Kairuki (KHEN), Kokushubira Kairuki.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...