Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Mshambuliaji kinara wa Young Africans SC, Fiston Kalala Mayele kwa sasa ni habari ya mjini baada ya kuwa Kiongozi katika orodha ya Wafungaji bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu huu wa 2022-2023.

Mayele kwa sasa tayari ameweka kambani mabao 10 akiwa kinara kwenye orodha hiyo ya Wafungaji, huku anayemfuata nyuma akiwa na mabao saba pekee, naye si mwingine ni Mshambuliaji wa Mbeya City FC, Sixtus Sabilo.

Mayele amefunga mabao mawili katika mfululizo wa michezo miwili ya Ligi hiyo, dhidi ya Dodoma Jiji FC, Mbeya City FC na amefunga mabao matatu (Hat-Trick) katika mchezo mmoja dhidi ya Singida Big Stars.

Katika orodha hiyo ya Wafungaji, Mshambuliaji wa Simba SC, Moses Phiri yupo nafasi ya tatu akiwa amefunga mabao sita sawa na Mshambuliaji wa Azam FC, Idriss Mbombo na Reliants Lusajo wa Namungo FC

Fiston amekuwa mwiba katika michezo mitatu ya mwisho kwa timu hiyo, baada ya kushindwa kufunga katika michezo takribani minne, dhidi ya Kagera Sugar, Geita Gold FC, KMC FC, Simba SC na Ruvu Shooting FC na hakubahatika kufunga katika michezo miwili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Mshambuliaji Moubarack Amza wa Coastal Union FC ana mabao matano wakati Kiungo Feisal Salum (Feitoto) wa Young Africans SC ana mabao manne sawa na Tariq Seif wa Mbeya City FC, Anuary Jabir wa Kagera Sugar FC, Matheo Anthony wa KMC FC.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...