Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Irene Isaka , akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na GIZ lililofanyika leo Novemba 24,2022 jijini Arusha.



Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Profesa Emmanuel Luoga, akisoma risala wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mbuyuwayu AICC, lililofanyika leo Novemba 24,2022 Jijini Arusha.



Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Profesa Suzana Augustino ni miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na GIZ lililofanyika leo Novemba 24,2022 Jijini Arusha.



Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)Dkt. Irene Isaka ,akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa masuala ya Teknolojia na Tehama kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Ujerumani na GIZ mara baada ya Ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na GIZ lililofanyika Leo Novemba 24,2022 Jijini Arusha.

.....................................

Na Mwandishi wetu, Arusha

WATAFITI vijana wanaofanya tafiti katika nyanja mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameagizwa kutoa matokeo ya tafiti zao ili kutatua changamoto zilizopo miongoni mwa jamii.

Hayo yamesemwa leo Novemba 24, 2022 jijini Arusha na Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)Dkt. Irene Isaka ,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na GIZ .

Amesema kuwa, endapo watafiti vijana wakitoa matokeo ya tafiti zao kwa jamii serikali za nchi za Afrika Mashariki (EAC ) zinaweza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi .

"Lazima sasa wasomi vijana wanapofanya tafiti zao wazitoe zisomwe ili serikali na jamii zichukue hatua katika kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa" amesema Dkt. Irene

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ,Profesa Emmanuel Luoga amesema kuwa CENIT@EA ni kituo cha Umahiri kinachojihusisha na masuala ya Kompyuta na Tehama ambacho kinahusisha nchi zote za Afrika Mashariki kwa lengo la kuhakikisha kuwa, masuala ya tafiti yanaibuliwa ili kutoa majibu sahihi ya changamoto za jamii na kuibua ajira.

Aidha, Prof Luoga ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi ya Ujerumani katika kuendeleza masuala ya elimu na tafiti kwa wanasayansi na wakufunzi kwa kipindi cha miaka saba tangu mwaka 2017.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki Profesa Gaspard Banyankimbona ameziomba serikali za nchi hizo kuweka fedha zaidi katika masuala ya tafiti, kwa lengo la kutoa majibu sahihi ya changamoto katika sekta mbalimbali za kijamii, ili kuwasaidia wasomi wanaofanya tafiti kutozifungia ndani bali wazitoe ili zisomwe na jamii ikiwemo idara mbalimbali na kuchukua hatua thabiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...