Na Mwandishi Wetu


KANISA la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam, limezindua kongamano liitwalo SHILO kama sehemu ya kumuenzi mwanzilishi wa Kanisa hilo, Hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare.

Uzinduzi wa kongamano hilo la siku nane ambalo hufanyika kila mwisho wa mwaka ulifanyika siku ya Jumapili mara baada ya Ibada kanisani hapo na Askofu Dunstan Maboya akiambatana na Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgetta.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kongamano hilo, Askofu Mgetta alisema kongamano hilo liliasisiwa na hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na limekuwa likifanyika kila mwaka hata baada ya kifo chake.

“Maombi ya SHILO yalikuwa ni maono ya Askofu wetu mwanzilishi hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na tumekuwa tukiyaendeleza mwaka hadi mwaka na makanisa yote ya Mlima wa Moto wamekuwa wakifanya maombi haya kila mwaka,” alisema

“SHILO ni majibu ya mwisho ya mtu ambaye amekata tamaa mfano ameshindwa kupata mtoto, ameshindwa kuolewa akija kwenye tamasha hili la siku nane la SHILO lazima jibu lake lipatikane,” alisema

Alisema wataendelea kuombea taifa liendelee kuwa na amani na kuondokana na majanga kama ukame na matatizo
  mbalimnbali yanayotokea kwenye jamii.

“Ili Kanisa liwe na amani lazima nchi iwe na amani kwa hiyo umekuwa wajibu wetu kuhakikisha tunaombea amani ya nchi mara kwa mara na tunamuombea Rais wetu Mungu aendelee kumpa afya njema aweze kuendelea kulikongoza vyema taifa letu,” alisema Askofu Rose

Naye Dk. Rose Rwakatare alisema kongamano la SHILO lilianza miaka 20 iliyopita katika Kanisa hilo lililoko Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

“Hili kongamano tunakuwa nalo kila mwaka na lilianzishwa na marehemu Askofu Dk. Getrude Rwakatare sisi tunaliendeleza kumuenzi na tunaahidi kuendelea kumuenzi situ kwa kongamano hili bali kwa kazi zote alizokuwa akizifanya,” alisema

Askofu Dunstan Maboya alisema marehemu Askofu Dk. Getrude Rwakatare aliweka misingi mizuri ya Kanisa na ndiyo sababu limekuwa likiendelea kutoa huduma ya kiroho hata baada ya kuondoka kwake.

“Namshukuru Rose Mgeta kwa kusimamia maono haya na kuhakikisha kazi ya Mungu inaendelea na nashukuru kwa mzigo mkubwaa aliona Rose kuombea taifa hili ni watu wachache wanaojitoa kuombea taifa lakini Rose na kanisa wamesimama kuombea nchi dhidi ya majanga kama ukame,” alisema Askofu MaboyaAskofu Dunstan Maboya kushoto akiongoza maombi ya ufunguzi rasmi wa kongamano la SHILO linalofanyia kila mwisho wa mwaka kwa makanisa ya Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar es Salaam. Anayefuata ni Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgetta.

Askofu Rose Mgeta wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Dar es Salaam akiwa na Askofu Dunstan Maboya kwenye uzinduzi wa kongamano la SHILO ambalo hufanyika kila mwaka.Askofu Dunstan Maboya na Askofu Mgeta wakiwa wamesimma kwaajili ya wimbo wa taifa kabla ya uzinduzi wa kongamano la SHILO linalofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Dar es Salaam.Askofu Rose Mgeta akimweleza jambo Askofu Dunstan Maboya wakati wa uzinduzi wa ufunguzi wa kongamano la SHILO linaloendelea kwenye Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam kama sehemu ya kumuenzi hayati Dk Getrude Rwakatare.Askofu Dunstan Maboya na Askofu Mgeta wakiwa na waumini wengine wakati wa maombi ya ufunguzi wa kongamano la SHILO linaloendelea kwenye Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam kama sehemu ya kumuenzi hayati Dk Getrude Rwakatare. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...