Njombe
WAKATI Tanzania ikiendelea kupinga ukatili wa kijinsia kupitia siku 16 za kukabilibiana na janga hilo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema hata vitendo vinavyofanywa na wanaume kwa wanafunzi mbalimbali vyuoni ikiwemo kuwanunulia simu,gari na hata kuwapangishia nyumba ni ukatili unaopaswa kupigwa vita.

Kissa ameeleza hayo katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika WILDAF unaofadhiliwa na shirika la kimarekani la maendeleo kimataifa USAIDS uliofanyika mkoani Njombe ukihusisha wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati takribani sita.

"Mnaposoma wapo wengine wananunuliwa vigali aina ya IST,wapo wengine wanapangishiwa nyumba kubwa,huu nao ni ukatili Kwasababu mwisho wa siku wanakunyima fursa ya kwenda kumiliki vya kwako"amesema Kissa Kasongwa

Vile vile amesema yeye binafsi kungekuwa na uwezekano angeshauri wazazi wasiweze kuwapeleka watoto shule za bweni wakiwa na umri mdogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakikabiliwa na ukatili mkubwa huku akipendekeza angalau watoto waanze wakiwa kidato cha kwanza na kama kukiwa na ulazima kwenda shule za bweni katika umri mdogo basi ziwekwe sheria na miongozo ambayo itaziangalia shule hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...