Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto’o alituhumiwa kumshambulia mtu mmoja aliyetajwa kuwa Mwandishi wa Habari wa nchini Algeria, kwa tuhuma za kudai kuwa alidhihakiwa na Mwandishi huyo nchini Qatar katika Michuano ya Kombe la Dunia.

Mnamo, Desemba 5, 2022 katika mchezo baina ya Brazil dhidi ya Korea Kusini, kwenye uwanja wa ‘Stadium 974’ Samuel Eto’o alisadikiwa kumshambulia mtu huyo baada ya baadhi ya picha za ‘video’ kuonyesha tukio hilo.

Eto’o amedai kuwa baadhi ya raia wa Algeria wamekuwa wakiwashambulia raia wa Cameroon kwa kile alichotaja kuwa raia hao wa Algeria wana uhasama na raia wa Cameroon tangu kuwatupa nje kwenye michezo ya kuwania kufuzu Michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar baina yao, katika michezo ya kanda ya Afrika.

“Mara nyingi nimedhihakiwa na Mashabiki wa soka Algeria bila sababu yoyote, baada ya sisi kucheza na wao, Machi 29, 2022 kwenye mji wa Blid tukifanikiwa kuwasukuma nje na sisi tukafuzu Michuano ya Kombe la Dunia”, amesema Eto’o.

Machi 29, 2022 timu ya taifa ya Cameroon iliitupa nje timu ya taifa ya Algeria katika Michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 kwa bao la ugenini baada ya kufungana jumla ya mabao 2-2, katika mchezo wa mkondo wa pili wa kufuzu Michuano hiyo, mchezo huo ulipigwa mjini Blida nchini Algeria kwenye dimba la Mustapha Tchaker.

Kutokana na tukio hilo la shambulizi kwa raia huyo wa Algeria, Samuel Eto’o ameomba radhi kwa umma baada ya kushindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akimshambulia mtu huyo. Eto’o ametoa rai kwa Mamlaka nchini Algeria kutazama hali hiyo ya uhasama kwa watu wa taifa hilo ili kuleta amani katika mchezo wa soka kabla ya hakujatokea maafa makubwa.

Cameroon waliitupa nje Algeria katika michezo ya kuwania kufuzu Michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwa jumla ya mabao 2-2, na Cameroon kufuzu kwa faida ya bao la ugenini.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Cameroon walifungwa bao 1-0 nyumbani kwao mjini Douala kwenye dimba la Japoma wakati mchezo wa mkondo wa pili, timu hizo zilitoka sare mabao 2-2 nchini Algeria


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...