Lions Club International wametoa msaada wa dawa zenye thamani TZS 15 Mil kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaogua saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema serikali imechukuwa nafasi kubwa kwenye matibabu ya watoto wanaougua saratani kwani matibabu yao ni gharama na yanachukuwa mda mrefu.

“Tunashukuru kwa msaada huu pia tunawakaribisha wadau wengine kuja kusaidia Hospitali yetu ya Taifa kwani uhitaji ni mkubwa kulingana na idadi ya wagonjwa”amesema Prof. Janabi.

Kwa upande wake, Bw. Mustansir Gulamhussein ( District Governor) amesema wameguswa kuja kutoa msaada wa dawa kwa watoto wenye saratani ikiwa ni malengo yao ambayo wamejiwekea.

“Swala la afya ni kipaumbele chetu sisi kama Lions Club International  watoto  ndio taifa la kesho hivyo ni jukumu letu kuwasaidia” amesema Bw. Mustansir.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...