Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MAONESHO ya Kitaifa ya YST 2022 ambayo ni Maalum kwa kuonesha kazi za kisayansi na Teknolojia yatafanyika Desemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam huku Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Maonesho hayo Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dkt.Gozibert Kamugisha ameeleza maandalizi yamekamilika na kwenye maonesho hayo kazi zitaoneshwa ni zile ambazo zimejikita zaidi katika masuala ya njia salama za utunzaji wa mazao ya kilimo na utunzaji wa mazingira
Pia matumizi endelevu ya rasilimali ya maji, dawa za asili na uboreshaji afya za binadamu, upatikanaji na uzalishaji wa nishati ya umeme, matumizi ya muziki katika ufundishaji wa somo hesabu mashuleni, matumizi ya mimea ya asili katika kuboresha uzalishaji wa maziwa ya ng’ombe na kutatua tatizo la udumavu wa ukuaji wa kuku.
"Mwaka huu idadi ya wanafunzi waliowasilisha maombi ya kufanya kazi za ugunduzi imeongezeka kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 1,143, kati ya idadi hiyo jumla ya kazi za utafiti na kisayansi 530 zimepatiwa usaidizi ambapo wanafunzi walioziandaa wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuziboresha na hatimaye kazi za kisayansi na ugunduzi 380 zimekamilika,"amesema.
Pia mesema mpango huu wa kuimarisha sayansi na ugunduzi kwa vijana unawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambaoni Karimjee Jivanjee Foundation/Toyota Tanzania huku akitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wadhamini ambao wamekuwa wakifanikishamaonesho hayo.
“Tunatoa shukrani kwa wadhamini wetu wengine kama Shell Exploration and Production Tanzania Limited (Shell Tanzania), Institute of Physics, Speedy Print, Exim Bank Tanzania Ltd, Concern Worldwide na COSTECH,” amesema Dk.Kamugisha alipokuwa akielezea Maonesho hayo ya kisayansi.
Wakati huo huo Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation Caren Rowland ameleeza namna ambavyo wamekuwa wakitoa ufadhili kwa wanafunzi ambao wanaibuka washindi wa YST pindi wanapomaliza masomo yao ya elimu ya juu "Hivyo mpaka sasa tumeshafadhili wanafunzi 37 na tunatarajia tena kuwadhamini wanafunzi wanne kwa mwaka huu wa 2022."Tutaendelea kuwa bega kwa bega na YST."
Aidha amesema kwamba wanafunzi ambao wamepata udhamini wamekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuwa madaktari, wahandisi, wanasayansi na wameonesha mabadiliko makubwa hapa nchini na hilo ni jambo ambalo hata wao wanalifurahia kuona jitihada wanazofanya zinakuwa na tija kwa Taifa la Tanzania.
Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dkt.Gozibert Kamugisha akisoma hotuba yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 4,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea Maonesho ya YST yatakayofanyika Desemba 8,2022 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. (kulia) Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland. 
Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland akisoma hotuba yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 4,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea Maonesho ya YST yatakayofanyika Desemba 8,2022 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dkt.Gozibert Kamugisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...