Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Nchini (JICA,) Naofumi Yamamura akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina hiyo na kueleza kuwa miaka 60 ya ushirikiano baina ya Tanzania na JICA wataendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na uchumi pamoja na kubadilishana ujuzi, Leo jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA,) Wanatabe Hideki akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina hiyo na kueleza kuwa bidhaa za Tanzania zinazokubalika katika soko la Japan ni pamoja na kahawa ya Tanzania, korosho na bidhaa za kilimo.Mshauri wa JICA Raymond Msofe akiendesha semina hiyoo.

 


*Kahawa ya ‘Kilimanjaro coffee’ korosho na bidhaa za kilimo kutoka Tanzania zatajwa kukubalika soko la Japan

*Watanzania 22,064 wanufaika  kupitia JICA

MIAKA 60 ya ushirikiano baina ya Serikali na Tanzania na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA,) imekuwa ya mafanikio makubwa hasa kwa JICA kuendelea kukua na kujitanua zaidi katika kusaidia katika kutoa misaada na kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na uchumi nchini  kwa kushirikiana na Serikali kwa kufuata vipaumbele vya watanzania.

Hayo yameelezwa leo na Mwakilishi Mkuu wa wa JICA nchini Naofumi Yamamura wakati wa semina maalum kwa waandishi wa habari pamoja na ziara ya kutembelea baadhi ya miradi iliyofadhiliwa na JICA uki wemo mradi wa kituo cha kupooza umeme kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na mradi wa daraja la juu ‘Mfugale Flyover’ lililopo Tazara jijini Dar es Salaam.

Amesema mahusiano baina ya Tanzania na Japan na Tanzania yalianza 1962 mara baada ya Uhuru wa Tanganyika na wataendelea kushiriki na kufadhili miradi mengi Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar kwa manufaa ya nchi hizo mbili ambapo watanzania 22,064 wamenufaika na programu za mafunzo zilizodhaminiwa na Serikali ya Japan huku Wajapan 1,679 wameshiriki program hizo za mafunzo na kunufaika na mambo mengi kutoka Tanzania ikiwemo utamaduni na lugha ya Kiswahili.

Aidha ameeleza ushirikiano huu uliudumu kwa miaka 60 na kutekeleza miradi mbalimbali  Tanzania ikiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la Salender 1980 utaendelea kudumu kwa manufaa ya watanzania.

Kwa upande wake Mwakilishi Mwandamizi wa (JICA,) Watanabe Hideki ameeleza kuwa kwa miaka 60 Serikali ya Japan kupitia JICA wameendelea kukuwa na kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia vipaumbele vya watanzania, huku Japan ikinufaika na mengi kutoka Tanzania ikiwemo kahawa ya Kilimanjaro Coffee, korosho na bidhaa za kilimo ambazo zinakubalika sana katika soko la Japan.

Amesema, kuanzia awamu ya kwanza ya uongozi wa Hayati. Julius K. Nyerere hadi katika awamu hii ya sita JICA inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya kijamii na maendeleo ikiwemo miradi ya ujenzi wa soko la samaki ‘Malindi Fish Market’  Zanzibar, ujenzi wa daraja la juu Gerezani, Dar es Salaam, ujenzi wa barabara mpya ya Bagamoyo ‘New Bagamoyo road’ Dar es Salaam sambamba na mradi mpya wa kuhimiza ujasiriamali na uvumbuzi kupitia Japan Project ‘NINJA na mradi wa kuhimiza usawa wa kijinsia ‘Ladies First’ mradi utakaoshirikisha sekta binafsi pamoja na mafunzo kupitia elimu na  kubadilishana teknolojia.

 Katika mradi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mhandisi mwandamizi wa Idara ya Usafirishaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO,) Kanda ya Mashariki Gwamaka Thobias amesema, kituo hicho kilichozinduliwa mwaka 2017 kwa ufadhili wa JICA kimekuwa msaada mkubwa katika uendeshaji wa hospitali hiyo kutokana na uhakika wa nishati ya umeme kwa muda wote.

‘’Taasisi nne zinanufaika na umeme kutoka katika kituo hiki ikiwemo Taasisi ya Moyo (JKCI,) Taasisi ya Mifupa (MOI,) Muhimbili pamoja na Chuo….nishati ni ya uhakika inafika moja kwa moja na kupoozwa katika kituo hiki na upatikanaji wa nishati ni wa uhakika na muda wote.’’ Amesema.

Mhandisi Gwamaka amesema JICA imesaidia kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo nyeti ambayo nishati haikuwa ya uhakika kutokana na umbali na miundombinu kupita katika eneo la Jangwani ambalo limekuwa likikumbwa na mafuriko.

Katika mradi wa barabara ya juu ya Mfugale ‘Mfugale Flyover’ ambayo ni Flyover ya kwanza kujengwa Tanzania mhandisi kutoka TANROAD Elisony Mweladzi amesema mradi huo uliojengwa kwa ufadhili wa JICA na kukamilika 2018 umeongeza ufanisi wa hali ya juu katika usafiri hasa wa abiria wanaotoka mjini na kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na maeneo ya Gongolamboto.

‘’Mradi huu umeongeza ufanisi mkubwa katika sekta ya usafiri, watu wanawahi Air port, na makazini ….kabla ya daraja hili magari yapatayo 21,557 yalikuwa yanapita kwa siku lakini baada ya mradi huu kwa takwimu za Novemba mwaka huu magari 39,300 yanapita katika daraja hili ikiwa ni ongezeko la asilimia 45.4.’’ Amesema.

Mhandisi Mweladzi ameishukuru JICA kwa ufadhili wa mradi huo na kueleza kuwa TANROAD inaona fahari kuwa na daraja hilo la juu la kwanza na la mfano Tanzania na kueleza kuwa kuna uhitaji wa madaraja nane zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Fire jijini Dar es Salaam. 

JICA ni shirika la maendeleo la kimataifa la Japan linalosimamia miradi yote inayofadhiliwa na Serikali ya Japan Tanzania, ikiwa na ofisi zaidi ya 90 ulimwenguni kote JICA Tanzania inafadhili katika ushirikiano wa kiufundi, mikopo ya masharti nafuu pamoja na misaada mbalimbali.




Baadhi ya Maofisa kutoka JICA wakiwasilisha mada katika semina hiyo.
Mwakilishi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA,) Watanabe Hideki (wa tatu kushoto,) akipata maelezo ya mtambo unaopooza na kusambaza umeme katika Hospitali ya Taifa Mhimbili kutoka kwa Mhandisi wa Idara ya Usafirishaji umeme Gwamaka Thobias (Kulia,) walipotembelea mradi huo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...