Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Tanzania Prisons SC wamekosa kiasi cha Shilingi Milioni 20 kutoka kwa Mdhamini wao Kampuni ya Silent Ocean Limited baada ya kupigwa bao 1-0 na Young Africans SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mtanange huo licha ya kufanikiwa kuzuia kwa dakika takribani 88’, Tanzania Prisons waliruhusu bao katika dakika ya 89’ kupitia kwa Kiungo Feisal Salum (Feitoto) ambaye alipokea ‘assist’ ya Farid Mussa baada ya kupokea mpira ulioshindwa kuondolewa na Walinzi wa Prisons katika eneo lao.
Tanzania Prisons SC wamepoteza mchezo huo, licha ya kuahidiwa kiasi hicho cha Tsh. Milioni 20, pia waliahidiwa kiasi cha Tsh. Milioni 10 endapo wangepata sare katika mchezo huo dhidi ya Wananchi, Young Africans SC.
Young Africans SC wakiwa na sherehe ya kufurahia ‘Unbeaten’ 49, wamerejea kilele mwa msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na alama zao 35 na michezo 14 ya Ligi hiyo, huku Tanzania Prisons wakibaki na alama zao 15 katika michezo 14.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...