NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja  amesema Serikali itaunda Kamati ya kuangalia migogoro ya mipaka na vijiji vinavyozunguka Msitu wa Hifadhi wa Bonde la  Wembere uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida.


Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa mipaka kwenye eneo la ardhioevu katika Kijiji cha Msai na Ujungu  mkoani Singida.

Amesema Kamati hiyo itaishauri Serikali endapo kuna umuhimu wa kurekebisha mipaka na kama eneo hilo  litafaa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu au la.

"Kuanzia leo tunaunda Kamati ambayo itajumuisha wataalam kutoka ngazi ya  Wizara,Mkoa na Wilaya na zoezi hilo litaanza mara moja na itapitia mipaka kwa kushirikiana na wananchi ili kuainisha mipaka halisi kwa kuzingatia ramani iliyopo ili kumaliza mgogoro huo," amesisitiza Masanja.

Mary Masanja amewataka wananchi hao kuzingatia sheria za kutovamia maeneo ya hifadhi na kuwa walinzi wa eneo hilo mara tathmini itakapokamilika. 

Kuhusu changamoto ya wafugaji  wanaopitisha ng'ombe katikati ya hifadhi kwa ajili ya kupeleka mifugo yao kunywa maji amesema, Serikali itaangalia namna iliyo bora ya kutatua changamoto hiyo ili wananchi wasiingiliane na masuala ya uhifadhi.

Sambamba na hilo amewataka wananchi waache tabia ya kukata miti hovyo na kukubaliana na mradi wa upandaji miti ulioletwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi wa Kata na vijiji kushirikiana na Kamati iliyoundwa wakati wa kupitia upya usahihi wa bikini zilizowekwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...