Mwenyekiti wa CHAVITA Selina Mlemba akizungumza na vyombo vya habari leo 1/12/2022 Jijini Arusha(Kiziwi )
Katibu Mkuu wa shirikisho la Vyama Vyama vya watu wenye ulemavu Jonas Lubalo(Haoni-kipofu)
Katibu Mkuu wa Kanisa la Viziwi Tanzania (CHAVITA)Mchungaji Joseph Hiza(Kiziwi)


Na Vero Ignatus,Arusha.


Leo ikiwa ni siku ya ukimwi duniani watu wenye ulemavu wamesema wamekuwa wakishindwa kujiepusha na janga hilo kwa urahisi kutokana na kukosa taarifa sahihi juu ya kujikinga na VVU na UKIMWI

Wameyasema hayo wakati wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Arusha Kuelekea siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu Duniani,kuwa kutokuwa na mawasiliano wamekuwa wakisahaukika na wengine kujikuta wakiingia matatani kwa kutokuwa na taarifa sahihi.

Akizungumza Katibu mkuu wa shirikisho vyama vya watu wenye ulemavu Jonas Lubalo wameiomba serikali kuweka mpango mkakati wa kuwapatia elimu ya mara kwa mara ili kuwaokoa na janga hilo sambamba na kuweka utaratibu ambao utawasaidia kwani wanaokwenda kupima afya zao wanahofia siri zao kuvuja kwani wengine hawaoni na wengine hawasikii

"Tumejikuta hatuna taarifa sahihi juu ya VVU na UKIMWI,hata wakati mwingine kwa sisi tusioona wala kusikia inakuwa shida sana kwenda kuoima kwani wakati mwingine unashikwa mkono wakati wa kupokea majibu anapokea mtu mwingine hivyo kunakuwa hakuna siri tena

Lubalo ametoa mfano wa janga la korona lilipoingia nchini kwamba walemavu wasiosikia na wale wasioona walipata tabu kwani walikuwa hawajui kinachoendelea walibaki wanaduwaa kwani mawasiliano ilikuwa changamoto kubwa kwao, na kuomba watu wajifunze lugha ya Alama ili iwe salama kwao.

Nae mwenyekiti wa CHAVITA Selina Mlemba amesema jambo hilo limekuwa likiwasumbua sana,nakusema anaamini Serikali ya ni sikivu na itasikia kilio chao na kuchukua hatua madhubuti.

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la watu wenye ulemavu Joseph Hiza amesema kuwa wanahitaji kupata mawasiliano ya kutosha pamoja na mkalimani wa lugha ya alama katika kupata mawasiliano kwani hata wao wana haki kama walivyo wananchi wengine

Aidha siku ya Ukimwi duniani inaadhimishwa huku ripoti mbalimbali zilizotolewa kuelekea siku hii kuhusu hali ya maambukizi ya Ukimwi duniani zinaonesha pengo kubwa la ukosefu wa usawa kati ya wanaopata huduma na wasiopata huduma na hali ni mbayĆ” zaidi kwa wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa , zaidi ya watu milioni wameambukizwa tangu mwanzoni mwa janga na zaidi ya watu milioni 40 walikufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.

Ikilinganishwa na siku za mwanzo wa janga, madawa ya kupunguza makali ya virusi sasa yanapatikana kila mahali lakini mafanikio sio sawa.


Umoja wa Mataifa unasema, huku 76% ya watu wazima kwa ujumla walipokea madawa hayo -antiretrovirals katika mwaka 2021, ni 52% pekee ya watoto (wa miaka kuanzia 0-14 ) waliopata tiba hiyo.

Kauli mbiu siku ya UKIMWI Duniani ya mwaka huu, “Imarisha Usawa.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...