Na Mwandishi Wetu


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uruguay, Luis Suàrez ameangua kilio uwanjani baada ya timu hiyo ya taifa kubaini kuwa itaaga mashindano ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, licha ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ghana.

Suàrez alianza kupagawa uwanjani na kujikuta akimwaga machozi wakati mchezo wao dhidi ya Ghana ukiendelea, wakati Korea Kusini imepata bao la pili dhidi ya timu ya taifa ya Ureno katika mchezo mwengine wa Kundi H uliopigwa kwenye dimba la Education City.

Wakati Uruguay wakiwa wanaongoza mabao 2-0 katika dimba la Al Janoub, Mshambuliaji huyo mtukutu, Suàrez alitolewa nje kwa kufanyiwa mabadiliko katika mchezo huo na kumpisha Mshambuliaji mwenza Cavani.

Michezo yote miwili ya Kundi hilo la H ilichezwa kwa wakati mmoja kwenye viwanja vya Al Janoub na Education City. Ureno tayari walijihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 Bora baada ya kuwa na alama sita kwenye michezo miwili ya mzunguko wa Kundi hilo.

Ghana walihitaji sare pekee dhidi ya Uruguay ili kufuzu hatua hiyo ya 16 Bora ya Michuano hiyo, lakini ilishindikana kwa kufungwa mabao 2-0, huku Uruguay walihitaji ushindi wa idadi kubwa ya mabao ili kujihakikishia nafasi hiyo.

Msimamo wa Kundi H, Ureno na Korea Kusini wamefuzu hatua hiyo ya 16 Bora, Ureno wakiwa na alama sita, Korea Kusini alama nne sawa na Uruguay wakati Ghana wakibaki na alama zao tatu pekee. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...