Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi nyingine za wizara ya Maliasili na Utalii (TTB, TFS) na kituo cha uwekezaji Tanzania -TIC limefanikiwa kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji  zilizopo nchini katika sekta mbalimbali. 

Wageni kutoka mataifa  mbalimbali waliofika nchini Qatar kwa ajili  ya mashindano ya kombe la Dunia, wameweza kupata taarifa muhimu  kwa karibu na kwa urahisi kabisa, zinazohusu vivutio vinavyopatikana Tanzania, huduma muhimu na njia za kuwafikisha.

 Aidha, Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Qatar alipata nafasi ya kukutana na washiriki wa maonesho haya na kufanya kikao  kilichojadili masuala ya kuendeleza utangazaji wa vivutio vyetu  ikiwemo kuwa na vipeperushi vya lugha ya kiarabu ambayo ndiyo inatumika zaidi nchi hapa.

  Aidha, ofisi ya ubalozi pia iliwakutanisha washiriki na wawekezaji walionesha nia ya kuwekeza nchini na kufanya nao mazungumzo. Ili kuongeza wigo wa matangazo na uhamasishaji,  washiriki kwa kushirikiana na ofisi ya Ubalozi, tumeweza kuratibu na kupata wanahabari ambapo Mh. Balozi aliweza kuzungumzia masuala mbalimbali yahusuyo utalii wa Tanzania na uwekezaji.  

Katika maonesho haya, Tanzania ni nchi pekee kutoka Africa iliyopewa nafasi ya kuwa na banda. Nchi nyingine zinazoshiriki ni Korea, Marekani na Uturuki.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...