TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Maonyesho makubwa ya sekta ya dawa na huduma za afya kutoka kwa wadau na wataalam wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Akizungumza na waandishi wahabari Jijini Dar es salaam, Mratibu wa Maonyesho kutoka kampuni ya Vegvoraus Thomas James amesema Maonyesho yatafanyika Disemba 14 hadi 16 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wazalishaji, wauzaji wa jumla na wafanyabiashara na wasambazaji wa sekta ya uchunguzi wa dawa, hospitali na watoa ushauri wenye ushawishi

mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki nchini Tanzania.

Aidha James ameongeza kuwa wanatarajia wadau takribani 90 kuhudhuria Maonyesho lengo likiwa ni kubadilishana teknolojia ya sekta hiyo ya Afya kutoka nchi mbalimbali pamoja na kuangalia fursa mbalimbali za vifaa tiba na madawa kutoka kwa nchi zilizoendelea kama nchini India.

Nae Katibu Mtendaji wa Katibu Mtendaji wa chama cha wanasayansi wa maabara Tanzania (Melsat) Brian peter ameongeza kuwa wadau mbalimbali kutoka nchini Tanzania watashiriki kwenye Maonyesho hayo hivyo wadau wanakaribishwa kutembelea Maonyesho hayo.

Peter amesema ni fursa kubwa kwa wadau wa afya nchini Tanzania wamepata kwani teknolojia inaenda kubadilika hivyo kuna wigo mkubwa kwenye sekta hiyo utapanuka na Maonyesho yatakapoisha Tanzania itakua nchi yenye neema na Maendeleo katika sekta ya Afya.

"Baada ya Maonyesho haya tunategemea kunifaika hasa wadau wa afya wa nchini Tanzania kuhakikisha tunatoa huduma za kiafya kwa weledi kwa kupata elimu kutoka mataifa mengine ambayo yatashiriki ".

Kwa upande wake Afisa wanachama wa chama cha wawezeshaji wanawake (TWCC) Cresensia Mbunda ameeleza namna Maonyesho hayo yanalenga kutoa fursa kwa wanawake katika kuhakikisha sekta ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wanashiriki kikamilifu kupata teknolojia mpya ya vifaa tiba,ushauri na usambazaji wa Madawa kutoka nchi husika zilitakazoshiriki Maonyesho hayo.

"Tunatarajia chama chetu kupata fursa mbalimbali kutoka kwa nchi zilizoendelea hususani katika sekta ya Afya namna wanavyotengeneza dawa ,upatikanaji wa vifaa mbalimbali mahospitali,huduma zao na vyanzo vya upatikanaji wa Madawa mbalimbali ambayo kwetu unakuta hayajafika."

Pia amesema wanawake watashiriki na watapata fursa ya kujifunza mengi ndani ya maonyesho hayo huku akiwakaribisha wanawake wengine kukimbilia fursa hiyo ya Maonyesho hayo.

Katibu mtendaji wa chama cha wanasayansi wa maabara nchini (Melsat) Brian peter akizungumza na waandishi wahabari Jijini Dar es salaam kuwaalika wadau wa sekta ya afya kushiriki katika Maonyesho ya makubwa ya sekta ya dawa na huduma za afya yanayotarajiwa kufanyika Disemba 14 hadi Disemba 16 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam
Mratibu wa Maonyesho kutoka kampuni ya Vegvoraus Thomas James akizungumza na waandishi wahabari na kuwaalika wadau wa sekta ya afya kushiriki kwenye Maonyesho ya sekta ya dawa na huduma za afya ambapo washiriki 90 wakiwemo mataifa mbalimbali yatashiriki lengo kubadilisha teknolojia mpya kwa nchi zilizoendelea

 Afisa wanachama wa chama cha wawezeshaji wanawake (TWCC) Cresensia Mbunda akizungumza na waandishi wahabari Akieleza kwa namna Maonyesho yamelenga kutoa fursa kwa watanzania kujifunza na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi  zitakazoshiriki ikiwemo nchi ya india ambao wanafanya vizuri katika sekta ya Afya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...