NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha kuwa wanatoa nafasi kwa watu wenye sifa kwenye kada ya manunuzi na ugavi.

Ndejembi ametoa agizo hilo jijini Arusha wakati akifungua kongamano la 13 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi.

Amesema kada hiyo imekua ikionekana haifai kutokana na waajiri kutoa ajira kwa watu ambao hawana taaluma na sifa jambo ambalo limekua likichangia kusababisha hasara kwa Serikali pindi kunapokua na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali nchini.

" Kada hii ni muhimu sana kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo tunahitaji kuwa na watu wenye sifa za kutosha na wenye taaluma, hivyo nitoe maelekezo kwa waajiri wa umma na taasisi mbalimbali kuzingatia vigezo pindi wanapokua wanaajiri.

Lakini pia nitoe wito kwenu wataalam wa ununuzi na ugavi kuhakikisha mnatekeleza majukumu yenu kwa weledi na kwa kufuata sheria zote zinazotakiwa kwenye taaluma yenu, nyinyi mkitekeleza majukumu yenu kwa weledi mnaisaidia pia Serikali kuokoa fedha nyingi zisipotee.

Wote ni mashahidi namna ambavyo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza miradi ya maendeleo kila kona na kwa wingi kwenye Nchi yetu, nyie kama wadau wa kubwa mnapaswa kutumia taaluma zenu kuhakikisha mnaleta matokeo chanya na kuepusha ubadhirifu mkubwa kwenye miradi ya Serikali," Amesema Ndejembi.

Naibu Waziri Ndejembi pia ameipongeza Bodi ya ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwa namna ambavyo wamekua wakitekeleza majukumu yao huku akiwasihi kutosita kuwachukulia hatua wataalam watakaokiuka maadili ya taaluma yao na kuisababishia Serikali ubadhirifu.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...