Na.Khadija Seif,Michuziblog 


MUITIKIO wa shindano Muasisi wa klabu ya Lugalo ya gofu, George Waitara "Waitara trophy" limekuwa na hamasa kubwa kwa mwaka 2023.

Akizungumza na Wanahabari Leo Januari 28,2023 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi,  Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema kuwepo kwa wadau wanaodhamini Mashindano ya Gofu inaleta hamasa ya kuongezeka kwa wachezaji wengi.

"Mimi ni mchezaji mpya wa Lugalo gofu lakini historia ya muasisi huyu naifahamu vizuri lakini pia niwakaribishe raia wote katika viwanja hivi kuwa ni vya kizalendo na vina nia ya dhati ya kuendeleza mchezo huu ili vipaji vingi viweze kuzaliwa.''

Hata hivyo Mhona ametoa pongezi kwa Kampuni ya Serengeti breweries kwa kupitia kinywaji cha John Walker kwa kudhamini shindano hilo kwa mwaka wa 3 mfululizo.

"Nawashukuru Kampuni ya Sengereti kupitia kinywaji chao Johnnie Walker kudhamini shindano hili, tangu walipoanza wachezaji wamezidi kuongeza."

Pia  ametoa wito kwa wazazi kuwasapoti  watoto wao kujifunza mchezo wa gofu na kuwa wachezaji bora kwa miaka ijayo.

Nae Meneja Masoko wa kampuni ya Serengeti breweries Irene Muganzi amesema lengo la kudhamini shindano hilo ni kuendeleza mchezo huo, pia kurudisha fadhila kwa jamii ambao ndiyo wateja wao.

"Tunajivunia kila mwaka idadi ya washiriki wanaongezeka, lakini tumeongeza wigo la kutoa udhamini katika mchezo kama klabu ya Kilimanjaro pamoja na kutoa udhamini mashindano mbalimbali lengo kuleta hamasa kwenye michezo nchini.

Kwa upande wa Nahodha wa Kabu ya Lugalo gofu Meja Japhet Masai amesema shindano la mwaka huu limejaza watu wengi kulinganisha na idadi ya miaka iliyopita. 

"Muitikio umekuwa mkubwa sana kwa shindano hili likifikia wachezaji 100, limetimiza mipango yake, amesema Masai.

Aidha,Masai ameeleza shindano hilo huwa na ushindani mkubwa tofauti na mashindano mengine kwani litafanyika mara 1 kwa mwaka .

"Shindano hili la siku moja, wachezaji wanapambana kwa lengo la kushindana kwa hali na mali kupata ushindi kutokana na shindano hili linafanyika mara 1 kwa mwaka .''
Mchezaji wa Shindano la "Johnie Walker Waitara Trophy" akiendelea na shindano hilo kwa kupiga mpira katika Viwanja vya Klabu ya Lugalo Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi  Meja Jenerali Ibrahim Mhona  akizungumza na Wanahabari Leo Januari 28,2023 katika Vijana vya Klabu ya Lugalo gofu Jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili katika shindano hilo la siku 1 ikijumuisha wachezaji 100 mdhamini mkuu akiwa Kampuni ya  Serengeti breweries  kwa mwaka wa 3 mfululizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...